Ronald Koeman kocha mkuu wa FC Barcelona akiwa ugenini ndani ya jiji la Kiev nchini Ukraine na kikosi cha FC Barcelona bila uwepo wa mshambuliaji wake nguli Lionel Messi, ameweza kupata ushindi wa goli 0-4 .

Mapema kabla ya kuondoka jijini Barcelona nchini Spain, Koeman alitoa taarifa kwa Umma amemuacha Messi ili apate muda mzuri wa kupumzika baada ya kuonesha kuwa na uchovu mwingi.

Koeman, Koeman Atamba Ligi ya Bingwa Bila Messi, Meridianbet

Ushindi wa FC Barcelona dhidi ya Dynamo Kyiv umeipa tiketi timu hiyo kuingia hatua ya 16 bora klabu bingwa Ulaya.

Magoli ya Barcelona yote yalifungwa kipindi cha pili pazia likifunguliwa na Sergino Dest mlinzi wa kulia wa timu hiyo na timu ya taifa ya Marekani. Dest alifunga goli dakika ya 52.

Koeman, Koeman Atamba Ligi ya Bingwa Bila Messi, Meridianbet

Dakika ya 57 mshambuliaji kutoka Denmark , Martin Braithwaite aliipatia Barcelona goli la pili . Dakika ya 70 tena Martin Braithwaite aliipatia Barcelona goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Deny Popov wa Kyiv ndani ya penalty box.

Koeman, Koeman Atamba Ligi ya Bingwa Bila Messi, Meridianbet

Pasi nzuri ya Jordi Alba dakika ya 90+2 ilimkuta Antoine Griezmann ambaye bila ajizi alitikisa nyavu za Dynamo Kyiv na kuandika goli la nne na la mwisho kwa FC Barcelona.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

15 MAONI

  1. Kiwango alichonacho Messi anaweza akapatikana mtu mwingine na akacheza vizuri nafasi hiyo tatizo barca waneona amna mtu anakayeweza kufit nafasi ya Messi na mpira ukachezeka wakashinda

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa