Kipa wa Aston Villa, Emiliano Martinez ameisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa UEFA Europa League Final baada ya kuifunga Freiburg mabao 3-0 licha ya kucheza akiwa na kidole kilichovunjika.
Martinez alipata jeraha hilo wakati wa mazoezi ya kupasha misuli moto kabla ya mchezo huo mkubwa uliochezwa Jumatano usiku, lakini aliamua kuendelea kucheza baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa timu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kipa huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye miaka 33 alionesha kiwango bora kwa kuokoa michomo miwili muhimu na kusaidia Aston Villa kutwaa taji lao la kwanza kubwa barani Ulaya tangu mwaka 1982 pamoja na kumaliza ukame wa miaka 30 bila ubingwa mkubwa.
Ushindi huo pia umeifanya Aston Villa kushinda taji lao kubwa la kwanza tangu walipotwaa Kombe la Ligi mwaka 1996.
Martinez amesema hakutaka jeraha hilo limzuie kucheza licha ya hofu ya kuongeza maumivu kabla ya Argentina kuanza kampeni ya kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia mwezi ujao.
“Leo nilivunja kidole wakati wa mazoezi ya kupasha misuli moto, lakini sikuona kama ni jambo baya,” alisema Martinez huku akicheka baada ya mchezo huo.

“Sijawahi kuvunja kidole kabla, na kila nilipojaribu kuudaka mpira kidole kilikuwa kinaenda upande mwingine. Lakini haya ni mambo ambayo lazima uyapitie,” aliongeza kipa huyo.


