Nimesikia maajabu mengi sana duniani ikiwemo mchanga unaotembea katika hifadhi ya taifa Ngorongoro. Nimesikia juu ya miti inayotembea ndani ya msitu mkubwa wa Amazon. Unajua bado siamini kama ipo chemchem inayotoa maji ya moto chini ya ardhi? Hii ni miujiza ya Mungu tu.

Mbona picha hapo juu ni ya Messi na stori inayoendelea hapa ni ya Mungu?? Je ninataka kumfananisha Messi na Mungu?? La! Kamwe Siwezi kushiriki dhambi ya kumuita Messi Mungu.

Messi, Messi Anavyotukumbusha Mungu Yupo, Meridianbet

Picha ya Messi akinyoosha mikono na kuangalia juu unaiona kila anapofunga. Ni kwasababu anakumbuka matatizo ya kukua aliyokuwa nayo utotoni. Barcelona wakamsaidia akapona. Lakini kamwe hajawahi kuamini kuwa Barca ndiyo wamemsaidia. Anaamini ni Mungu tu. Licha ya hayo anaamini ni Mungu aliyempa kipaji, si ujanja wake.

Hiyo ndiyo sababu haya maandiko yamekuja muda huu. Hiyo ndiyo sababu picha ya Lionel Messi ipo hapo juu. Wakati unasherekea mwaka huko ulipo, kumbuka kumshukuru Mungu alipokutoa. Labda asubuhi nitaweka picha ya Sadio Mane akisujudu halafu nitaandika mengine. Huyu Messi wa leo ni nani?

Messi, Messi Anavyotukumbusha Mungu Yupo, Meridianbet
Sadio Mane Akisujudu Uwanjani

Maajabu ya miguu yake yanaanza kusimuliwa Paris kwenye tuzo za ‘Ballon d’or’ 2005. Gaucho alipopewa tuzo ya mchezaji bora wa dunia alisema, “Hii tuzo inasema mimi ni bora duniani, ila ninawaambia ukweli mimi sio bora hata ndani ya Barcelona.”

Messi, Messi Anavyotukumbusha Mungu Yupo, Meridianbet

Dunia ilimuona Gaucho kichaa. Yaani kuna mchezaji bora Barcelona zaidi yako? Nani? Xavi Hernandez au Samuel Eto’o. Si dokta Kashushu Leakey wala mzee Habibu Msonjo aliyeelewa maneno yale.

Ila Gaucho alishamtazama Messi pale La Masia, kisha akacheza naye El Clasico akamuona mtoto wa miaka 17 anavyopangua ukuta wa Sergio Ramos, Ivan Helgera, Roberto Carlos na golini alikuwepo Iker Casilas, Gaucho akakubali huyu dogo ni ‘moto na mkaa wake’.

Messi, Messi Anavyotukumbusha Mungu Yupo, Meridianbet

Leo hii mikono ya Messi imenyanyua makombe zaidi ya 33. Miguu yake imevunja rekodi ya mabao ya mfalme wa soka Pele. Shingo yake imetundika medali zaidi 40. Sura yake imepigwa picha na ballon d’or sita. Kabatini kwake ana tuzo zaidi ya 80 na jezi zake mbili tu, Barcelona na Argentina.

Messi, Messi Anavyotukumbusha Mungu Yupo, Meridianbet


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

Messi, Messi Anavyotukumbusha Mungu Yupo, Meridianbet

SOMA ZAIDI

23 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa