Lilikuwa pambano lao la mwisho kuwaaga mashabiki wa ngumi ulimwenguni. Umri wao ulishaenda na hakukuwa na uwezekano wa wao wawili kukutana tena.

Hii ilikuwa ni mara ya tatu wanakutana, mara ya kwanza Joe Frazier alishinda, mara ya pili Muhammad Alli alishinda, hili pambano la mara ya tatu lilikuwa la kumaliza ubishi, nani mkali kuliko mwenzake?

Sitaki kujua sana kuhusu ushindi wa Muhammad Alli, yeye mwenyewe alikiri kuwa Frazier alikimbia pambano sekunde kadhaa kabla yake. Zilipigwa ngumi, yalitupwa mawe, yakapigwa masumbwi. Frazier akatupa taulo raundi ya mwisho.

Ronaldo, Ronaldo na Messi Walivyoturudisha Manilla, Ufilipino, Meridianbet

Watu waliburudika, watu walifurahia, watu wakachekelea. Kawaida ya binadamu tunaongozwa na hisia sana. Akili ziliporejea watu wakagundua haukuwa wakati wa furaha bali huzuni. Ipo sababu gani ya kufurahi wakati hawatalishuhudia pambano la Frazier na Alii tena?

Habari ya Ufilipino Manilla iliisha hivo, Frazier na Alli hawakuwahi kurudi ulingoni kuzichapa pamoja tena. Wakaiacha dunia katikati ya majonzi na masikitiko. Kwa sasa hawa wote wamelala na imebaki stori tu. Haijawahi kutokea vita ya masumbwi kama ile tena.

Baada ya upinzani kwa zaidi ya miaka 10, UEFA wakaturudishia tena mechi ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Huyu Messi ana miaka 33, Ronaldo yeye ana miaka 35. Si wale tena waliokausha makoo ya mashabiki wao dunia nzima.

Ronaldo, Ronaldo na Messi Walivyoturudisha Manilla, Ufilipino, Meridianbet

Si wale tena wenye tuzo 11 za wachezaji bora wa dunia kati yao. Si wale tena! Mara hii ni kama wamekuja kutuaga. Ni kama wamekuja kutupa kwaheri. Hatutawaona tena, hata tukiwaona hatutawaona tena wale walio bora.

Ronaldo, Ronaldo na Messi Walivyoturudisha Manilla, Ufilipino, Meridianbet

Pengine tunaiona mechi yao ya mwisho, pengine hatutapata vita kama hii yao tena. INAUMA. Kama ilivokuwa Manilla, soka litaendelea ila historia yao itadumu🙏.


MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!

Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!

Ronaldo, Ronaldo na Messi Walivyoturudisha Manilla, Ufilipino, Meridianbet

SOMA ZAIDI

21 MAONI

  1. Baada ya upinzani kwa zaidi ya miaka 10, UEFA wakaturudishia tena mechi ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Huyu Messi ana miaka 33, Ronaldo yeye ana miaka 35. Si wale tena waliokausha makoo ya mashabiki wao dunia nzima.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa