Shirikisho la Soka barani Ulaya, UEFA, limetangaza kuitoza faini klabu ya Benfica kiasi cha euro 40,000 (takribani dola 46,250) kufuatia vitendo vya “ubaguzi na/au unyanyasaji” vilivyofanywa na mashabiki wake wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi uliopita.
Mbali na adhabu hiyo, UEFA pia imeitoza Benfica faini ya euro 25,000 kwa mashabiki kurusha vitu uwanjani na euro 8,000 kwa matumizi ya mwanga wa laser, huku kocha msaidizi Pedro Machado akisimamishwa kwa mchezo mmoja kutokana na utovu wa nidhamu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Lisbon, Real Madrid iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lakini tukio hilo lilitawaliwa na malalamiko ya nyota wa Madrid Vinicius Jr aliyedai kutukanwa kwa maneno ya kibaguzi na mchezaji wa Benfica Gianluca Prestianni.
Hata hivyo, Prestianni pamoja na klabu yake ya Benfica walikanusha vikali tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa mchezaji huyo hakutoa kauli yoyote ya kibaguzi kama ilivyodaiwa na Vinicius Jr.
Baada ya tukio hilo, UEFA ilifungua uchunguzi rasmi na kumfungia kwa muda Prestianni kushiriki mchezo wa marudiano uliochezwa Madrid, ambapo Real Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 3-1.
Aidha, UEFA imeionya Benfica kwa kuiwekea adhabu ya kufunga sehemu ya uwanja wake katika mchezo mmoja wa nyumbani, adhabu ambayo imesimamishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kama hatua ya tahadhari dhidi ya matukio ya baadaye.

