Xavi na Iniesta Walivyonionyesha Ajabu Lingine la Dunia EURO 2012

Italy wanapigwa 4-0 ndani ya Kyiev Ukraine. Wameshindwa kabisa kujibu maswali magumu wanayoulizwa na Hispania. Watafanya nini mbele ya watoto wanaowaka moto mguuni? Katikati yupo Sergio Busquets, Xavi Hernandez, David Silva na Xabi Alonso. Utawaambia nini? Hapo Andres Iniesta amesogezwa mbele, Italy wamedanganywa ni mshambuliaji. Watoto wa Hispania hawaelewi kitu, wanapika tu sambusa uwanjani. Wanagonga tu. Hiyo Hispania, acha kabisa.

Hispania walikuwa na kiburi cha binadamu mmoja katikati ya dimba aliyezibeba akili zao, akaibeba falsafa yao na akabeba ramani yao. Alipiga pasi zaidi ya nusu za pasi walizopiga Italia. Bado alitoa assist mbili. Alikuwa kitanzi kwenye shingo ya Italia. Sorry, namzungumzia Xavier Hernandez Creus.

Baada ya bao la Juan Mata, Ilibidi Iker Casilas asogee hadi katikati ya uwanja kuwaombea Italy msamaha. Casillas akamnong’oneza Xavi, “Hii ni Italy, mabingwa wa dunia mara nne, isitoshe wana Andre Pirlo katikati ya uwanja na gwiji Gianluigi Buffon langoni, sitataka kuwaona wakifungwa tano, tafadhali inatosha. Wasimamishe vijana”. Hiyo ndio ikawa ‘pona’ ya Italy.

Usisahau hiyo ni fainali ya ‘EURO 2012’, wanaitetea tena kwa mara ya pili. Ni hapahapa Kyiev walivunja rekodi ya kupiga pasi nyingi katika mchezo mmoja. Wakati wanawakung’uta Ireland katika mchezo wa makundi, Hispania walipiga pasi 857, Xavi na rafiki yake Iniesta wakipiga nyingi zaidi ya timu nzima ya Ireland. Iniesta akawa mchezaji bora wa mashindano, ila Xavi alikuwa mchezaji bora mashindano yaliyopita ya 2008. Wakabadilishana tuzo kama walivozoea kubadilishana namba za jezi. Vaa nane klabuni, mimi niivae timu ya taifa. Wale watu.

Muulize hata Frank Lampard anawajua. Alipoulizwa kiungo mgumu kuwahi kukutana nae, alishindwa kuchagua akasema tu Xavi na Iniesta. Sijui yupi mgumu zaidi, ila hao wawili. Sijawahi kuona wachezaji wanaoelewana uwanjani kama wao. Huwezi kuwasogelea, huwezi kuwakaba, huwezi kuwakimbia, wanakuchanganya tu. Hadi sir Alex Ferguson analijua balaa lao. Wakati Barca wanampiga 2011..

ITAENDELEA..


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

33 Komentara

    duh!!!mambo moto

    Jibu

    Wako vizuri sana

    Jibu

    Viungo Bola kuwahi kutokea dunian

    Jibu

    Aisee! Ilkua balaa

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Ahsant sana meridianbet kwa makala

    Jibu

    Viungo bora kabisa wapo vizuri sana na wanaviwango vya hali ya juu

    Jibu

    Waliofanya vzur sana kipind kile ila still now wamechoka

    Jibu

    Wapo vizur hatar!!

    Jibu

    Wako vizuri sana

    Jibu

    walikuwa nguli sana kipindi iko

    Jibu

    Viungo bora duniani

    Jibu

    Wako vizuri sana

    Jibu

    Safii sana kwao

    Jibu

    Update nzuri!

    Jibu

    Wapo vizuri hao

    Jibu

    Ilikuwa raha kuona soka lile la spain kama vile play station#meridianbettz

    Jibu

    Duuu wako bomba sana

    Jibu

    Viungo makini sana hawa walikinukisha kipindi hik

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Kipindi hicho ndio walitamba

    Jibu

    Duh mambo yalikuwah ni moto Sana enzi hzo

    Jibu

    Ilikua nomaa

    Jibu

    Viungo bora kuwahi kutokea pale spain

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Waliofanya vzur sana kipind kile ila still now wamechoka

    Jibu

    Walifanya makubwa kwenye ulimwengu wa soko sema hawakuwa na bahati

    Jibu

    Wameweka history nzuri

    Jibu

    Kizazi cha Xavi na Iniesta bado hakina warithi ndani ya Spain

    Jibu

    viungo bora hawajai kutokea duniani

    Jibu

    Balaaa sana.

    Jibu

    Walikuwa vizuri ila hasaivi hana kitu kabisa

    Jibu

    Hawa jamaa wote wakali

    Jibu

Acha ujumbe