Katika mchezo wa NBA All Stars, mchezaji nyota wa Milwaukee Bucks – Giannis Antetokoumpo alionesha umwamba wake na kung’ara akiwa na Team LeBron.
Akiwa kwenye timu moja na wachezaji mahiri kama Damian Lillard, Stephen Curry na Chris Paul. Giannis hakuwa na majukumu makubwa kwenye timu zaidi ya kuonesha uwezo wake uliomfanya kuwa MVP wa mchezo huo.
Team LeBron walikuwa wakipambana na Team Durant katika mchezo uliochezwa jijini Atalanta, Marekani na team LeBron kuibuka kidedea kwa matokeo ya pointi 170-150.
Antetokoumpo alikuwa kinara wa mchezo huo kwa kupachika pointi 35 ikiwa ni sambamba na kupachika mipira 16 kati ya 16 aliyolenga kikapu.

Baada ya mchezo, Antetokoumpo alizungumzia uwezo aliouonesha kwenye mchezo huo ambapo pia alinukuliwa akisema kuwa hakuwaza kama anaingia mchezoni kutafuta tuzo ya MVP, kwake ilikuwa kufurahia mchezo na tuzo imekuja kama nyongeza tu.
“[Tuzo ya MVP] Haikuwa akilini mwangu. Nilikuwa ninataka tu kucheza. Unapokuwa umezungukwa na watu kama Damian Lillard, Stephen Curry na Chris Paul inakuwa ni rahisi zaidi.

“Hakuna mtu alikuwa ananiogopa, nilikuwa ninacheza 1 vs 1, hakuna kukabana wawili wawili.
“Kama unajisikia vizuri, na mimi ninajisikia vizuri basi inakuwa vizuri. Nilikuwa ninafurahia mchezo na kurusha mipira mingi kadiri nilivyoweza.” alisema Antetokoumpo.
Nilijua tu giannis yuko poa sana
Safi sana
Nice
Daaa hongera yake
Safi
Kijanja yuko vizuri hongera yake
Umekuwa uwili wennye faida kwa Lakers
Safii sana
Gud
Hongera G
Good