Miami Heat wamefanya moja ya usajili mkubwa zaidi katika historia ya NBA baada ya kumchukua nyota wa Milwaukee Bucks, Giannis Antetokounmpo, katika biashara kubwa iliyotikisa ligi hiyo. Mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya MVP na mchezaji wa All-Star mara 10 sasa ataungana na Bam Adebayo huku Heat wakionyesha wazi nia yao ya kurejea kwenye mbio za ubingwa.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Miami wamewapata Giannis pamoja na Bobby Portis, huku Milwaukee Bucks wakipokea Tyler Herro, Kel’el Ware, Jaime Jaquez Jr., Kasparas Jakucionis, chaguo la 13 la NBA Draft ya 2026, pamoja na chaguo za raundi ya kwanza za mwaka 2031 na 2033, haki ya kubadilishana chaguo mwaka 2030 na chaguo la raundi ya pili mwaka 2033.
Kwa Miami, huu ni mwendelezo wa utamaduni wao wa kuwinda mastaa wakubwa. Klabu hiyo iliwahi kuwasajili Shaquille O’Neal mwaka 2004 na baadaye kuunda kikosi cha ndoto kilichowajumuisha LeBron James, Chris Bosh na Dwyane Wade mwaka 2010. Sasa ni zamu ya Giannis kupewa jukumu la kuiongoza Heat kwenye safari ya kutafuta ubingwa mwingine.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa upande wa Milwaukee Bucks, biashara hiyo inaashiria mwanzo mpya. Baada ya kuachana na kocha Doc Rivers na kukosa kikosi cha ushindani, viongozi wa Bucks wameamua kuanza upya kwa kujenga timu kupitia vipaji vipya na chaguo nyingi za draft walizopata kutoka Miami. Hii inafunga rasmi ukurasa wa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi katika historia ya klabu hiyo ambaye aliiongoza Bucks kutwaa ubingwa wa NBA mwaka 2021.

Giannis mwenyewe amekuwa akizungumza kwa heshima kubwa kuhusu utamaduni wa Miami Heat kwa miaka mingi. Sasa atakuwa sehemu ya mfumo huo akiwa sambamba na Bam Adebayo, ambaye Heat walikataa kabisa kumjumuisha kwenye mazungumzo ya biashara hiyo.


