Mchezaji wa Milwaukee Bucks – Giannis Antetokounmpo amerejea kwenye vichwa vya habari baada ya kuwaangusha vigogo wa NBA kwenye mchezo dhidi ya LA Clippers.

Bucks walikuwa uwanjani Jumapili usiku kupambana na Clippers inayoongozwa na wachezaji wenye majina makubwa kwenye NBA akiwemo Kawhi Leonard.

Baada ya vuta n’kuvute ya muda mrefu, Antetokounmpo alifanikiwa kupachika pointi 36 na kucheza mipira 14 iliyokufa. Giannis aliendelea kuwa mwiba mkali kwa Leonard na wenzake katika kipindi cha 4 ambapo alipachika pointi 9 zilizowapa ushindi Bucks kwa pointi 105-100.

Giannis Antetokounmpo, Giannis Antetokounmpo Awaangusha Vigogo NBA., Meridianbet
Antetokounmpo akiwapatia pointi Bucks

Giannis Antetokounmpo anakuwa ni mchezaji wa kwanza kwenye historia ya Bucks kupachika zaidi ya pointi 35 kwenye michezo 4 mfululizo, historia hii ilikuwa ikishikiliwa na Kareem Abdul-Jabbar mwaka 1973.

Baada ya kupoteza michezo 5 mfululizo, Bucks wamerejea kwenye ushindi wakiwa wameshinda michezo 5 mfululizo na sasa wanashika nafasi ya pili nyuma ya Philadelphia 76ers kwenye msimamo wa NBA- Eastern Conference.

Matokeo ya michezo iliyochezwa Jumapili:
Los Angeles Lakers 117-91 Golden State Warriors, Memphis Grizzlies 133-84 Houston Rockets, Miami Heat 109-99 Atlanta Hawks, New York Knicks 109-90 Detroit Pistons, Boston Celtics 111-110 Washington Wizards, Charlotte Hornets 127-126 Sacramento Kings na Phoenix Suns 118-99 Minnesota Timberwolves


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Huhitaji kufikiria mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

Giannis Antetokounmpo, Giannis Antetokounmpo Awaangusha Vigogo NBA., Meridianbet

  CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa