Mambo yanazidi kunoga kunako nusu fainali ya Eastern Conference. Kevin Durant (KD) ameendelea kuwa mwiba kwa vijana wa Milwaukee Bucks.

Brooklyn Nets walikuwa wakichuana na Bucks kwa mara ya 2 katika fululizo wa michezo 7 ya nusu fainali. KD alimaliza mizunguko mitatu kwa kupachika jumla ya pointi 32 kati ya 125 zilizowazidi Bucks ambao waliambulia pointi 86 pekee.

Licha ya kumkosa James Harden ambaye aliumia kwenye mchezo wa kwanza, Kevin Durant alihakikisha wanaendelea walipoishia kwenye mchezo wa kwanza na sasa wanaongoza kwa matokeo ya 2-0 dhidi ya Bucks.

Kevin Durant
James Harden (kushoto) akishangilia na KD (kulia)

Sambamba na kupachika pointi 32, KD alitoa pasi 6 za magoli akisaidiana na nyota mwenzake, Kyrie Irving ambaye alipachika pointi 22.

Mchezo wa 3 itakuwa ni safari ya Nets kuwafata Bucks baada ya kushinda michezo miwili wakiwa nyumbani. Mshindi kati ya Nets vs Bucks, atachuana na mshindi kati ya Atlanta Hawks vs Philadelphia 76ers (1-0) katika mchezo utaompatia mshindi wa Eastern Conference nafasi ya kucheza fainali ya NBA mwezi ujao.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa