Knicks Waichapa Cavaliers Na Kuingia Fainali Ya Nba

New York Knicks wameandika historia kubwa baada ya kuifunga Cleveland Cavaliers kwa ushindi wa kishindo wa 130-93 kwenye Game 4, wakikamilisha sweep ya 4-0 na kutinga fainali za NBA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1999. Ushindi huo umewafanya mashabiki wake kuanza kuota tena ndoto ya ubingwa ambao haujafikiwa tangu 1973.

Knicks Waichapa Cavaliers Na Kuingia Fainali Ya Nba

Mchezo huo haukuwa na ushindani mkubwa baada ya Knicks kuanza kwa kasi ya ajabu, wakiongoza kwa pointi 12 baada ya robo ya kwanza na kuendeleza moto huo kwa asilimia 56 ya mashuti yaliyopigwa ndani ya dakika 12 za mwanzo. Uongozi wa 20-0 uliwapoteza kabisa Cavaliers, na kabla ya mapumziko Knicks walikuwa tayari wameshika mchezo mikononi.

Nyota wa kikosi hicho Jalen Brunson alicheza kwa kiwango cha juu tena, akimaliza na pointi 15 na pasi 5 za mabao, huku akipata heshima ya kuwa MVP wa Finali za Eastern Conference kwa kura zote. Mashabiki walikuwa wakimshangilia kabla hata mchezo kumalizika, ishara ya jinsi alivyoongoza timu hiyo kwenye mafanikio makubwa.

Knicks Waichapa Cavaliers Na Kuingia Fainali Ya Nba

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Karl-Anthony Towns aliongeza nguvu kwa pointi 19 na rebound 14, huku OG Anunoby akimaliza na pointi 17, na kuwafanya waonekane timu yenye uwiano mzuri wa mashambulizi na ulinzi. Cavaliers upande wao walitegemea Donovan Mitchell aliyefunga pointi 31, lakini hakukuwa na msaada wa kutosha kuzuia mafuriko ya Knicks.

Knicks Waichapa Cavaliers Na Kuingia Fainali Ya Nba

Sasa Knicks wanasubiri mshindi kati ya San Antonio Spurs na Oklahoma City Thunder, huku wakipata muda wa kupumzika kabla ya fainali hizo zitakazoanza Juni 3. Baada ya mfululizo wa ushindi 11 mfululizo, Knicks wanaingia fainali wakiwa na morali kubwa na ndoto ya kuandika historia mpya ya NBA.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.