LA Lakers Mabingwa wa NBA 2019/20

Kunako anga la mpira wa kikapu, LA Lakers wametwaa ubingwa wa NBA 2019/20. Ushindi katika mchezo wa 6 umewatosha Lakers kubeba ubingwa baada ya miaka 10.

Ama kweli kukata tamaa ni jambo ambalo halipaswi kupewa nafasi, kuamini katika muda muafaka ni kitu sahihi. LA Lakers wamesugua benchi kwa miaka 10 bila taji la NBA na sasa ukata wao umemalizika 2019/20.

LeBron James na Anthony Davis watabaki kuwa mashujaa wa LA Lakers vizazi na vizazi baada ya kuisaidia timu hiyo kubeba taji la NBA msimu huu.

Uelewano wao uwanjani na kujituma kwao kulikuwa ni chachu ya mafanikio ya Lakers msimu huu. Walicheza kwa kujiamini na kuisaidia timu yao kwa ujumla, katika kila hali walionekana kuwa pamoja na kuhakikisha lengo lao linatimia.

Ushindi wa pointi 106-93 dhidi ya Miami Heats, ulitosha kuwapa Lakers taji la 17 la NBA. LeBron James akajibebea taji la Mchezaji bora wa fainali (Most Valuable Player -MVP) baada ya kupachika pointi 28, alitoa pasi 10 za magoli na kucheza mipira 14 iliyokufa.

Ushindi huu wa LA Lakers, umewapa nafasi ya kuwa sawa na Boston Celtics kama timu zilizobeba mataji mengi ya NBA.

Wachezaji wa LA Lakers wakishangilia ubingwa wa NBA.

“Hii inamaana kubwa sana kwenye timu hii Wakati ninajiunga na timu hii, nilimwambia raisi (Jeanie Buss) ninakwenda kuirudisha timu katika nafasi yake inayostahili.

“Tunahitaji heshima yetu. Rob [Pelinka] anahitaji heshima yake,  kocha [Frank] Vogel anahitaji heshima yake, timu yetu inahitaji heshima yake na mashabiki wote wa LA Lakers wanahitaji heshima zao.

“Na mimi pia ninahitaji heshima yangu.” alisema LeBron James.


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

18 Komentara

    nilijua tu hamtoniangusha na mmefanya kweli pongezi kwenu vijana wa NBA nawakubali tangu mwanzo

    Jibu

    Hanajituna sana lebron james pale la Lakers nafasi yake kama messi Barcelona

    Jibu

    Pongezi kwao

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

    Pongezi zao Lakers

    Jibu

    Wanasitahili pongezi sana

    Jibu

    Safi lakers

    Jibu

    Lakers walikuwa wazuri toka mchezo ulivyoazs

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

    Pongezi kwao lakers

    Jibu

    Wamestahili maan wamekua Bola msim huu

    Jibu

    Pongezi kwao

    Jibu

    Bravo LA LAKERS, Bravo Lebron James. Tangu asitaafu Kobe Bryant hakupatikana mtu mwenye uwezo aina yake kuirudisha timu kwenye enzi za ushindi

    Jibu

    Weee hongera sana LA LAKERS kazi nzuri

    Jibu

    Lakers wamestahili, Pongezi kwao

    Jibu

    Safi sana Lakers

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

    Hongera yaoo

    Jibu

Acha ujumbe