Kama ilivyo kwa Liverpool kwenye EPL. Kunako NBA, LA Lakers hali sio shwari kutokana na muenendo mbaya wa matokeo kwa siku za karibuni.
Lakers walikuwa uwanjani kupambana na vinara Uttah Jazz. Huu ni mchezo ambao uliwakutanisha bingwa mtetezi wa NBA (Lakers) dhidi ya wanaowania ubingwa msimu huu (Jazz).
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa baada ya raundi zote 4 kuchezwa, LA Lakers walikuwa wameshapigwa kwa pointi 89-114.
Licha ya LeBron James kuibuka kinara wa mchezo huo kwa kupachika pointi 19, hazikuwatosha Lakers kujinasua kwenye mfululizo kwa kupoteza michezo 3 kabla ya kukutana na Jazz.
Jazz anaendeleza umwamba msimu huu akiwa ameshinda michezo 22 kati ya 24 aliyocheza mpaka sasa msimu huu. Timu hii imeendelea kufanya vizuri kwenye uwanja wake wa nyumbani wakiwa na wastani wa kushinda michezo 15-2.
Matokeo ya michezo ya NBA iliyochezwa Jumatano usiku:
Atlanta Hawks 127-112 Boston Celtics, Golden State Warriors 111-107 Indiana Pacers, Cleveland Cavaliers 112-96 Houston Rockets, New Orleans Pelicans 128-118 Detroit Pistons, Oklahoma City Thunder 102-99 San Antonio Spurs, Miami Heat 116-108 Toronto Raptors, Chicago Bulls 133-126 Minnesota Timberwolves na Charlotte Hornets 124-121 Phoenix Suns
TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET
BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.
warda
Pole yao wamezidi