Kunako NBA, michezo ya mtoano (Play-Offs) inaendelea kushika kasi. LA Lakers walikuwa na wakati mzuri dhidi ya Portland Trail Blazers.
Blazers walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuambulia kipigo cha pointi 135- 115 katika mchezo uliochezwa mjini Orlando – Marekani.
LeBron James alifunga pointi 30 na kuisaidia Lakers kupata ushindi wa 3-1 katika mzunguko wa kwanza wa Western Conference Play-Offs.

LA Lakers yatoaheshima kwenye kumbukumbu ya Kobe Bryant.
Bryant na binti yake Gianna ni kati ya watu 9 waliofariki katika ajali ya helikopta mwezi Januari 2020. Siku ya jumatatu ilipewa jina la “Mamba Day” na NBA kwasababu namba 24 na 8 ni namba alizokuwa anazitumia uwanjani gwiji huyo [Kobe Bryant].
“Nilipoangalia ubao wa matokeo ukisoma 24-8, nilisema sawa, yupo hapa. Ninajivunia timu yangu, kwa namna tulivyocheza. Nimebarikiwa sana na kupewa heshima ya kuendelea kumuenzi Kobe Bryant na Gigi Bryant na watu wote waliokuwepo kwenye ajali ile.” amesema LeBron James.
Lakers walivaa jezi maalumu ya rangi nyeusi na njano kama ishara ya kumuezi Kobe Bryant ambaye angekuwa anasheherekea miaka 42 ya kuzaliwa Jumapili hii.
Akiwa bingwa wa NBA mara 5, Bryant aliitumikia LA Lakers kwa miaka yake yote kama mchezaji. Ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye ligi hiyo kutumia namba mbili za jezi akiwa na timu moja kwa zaidi ya miaka 10.
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


magdalena
kobe alikuwa na mchango mkubwa sana katika mchezo wa kikapu na ataendelea kukumbukwa daima aendelee kupumzika kwa amani
Ernest
Lakers chama langu waendelee kukaza buti tuu
Lydia Emmanuel Magoti
Kobe alikuwa na mchango mkubwa kwenye Lekers lazima wa mpe eshima nakukumbukwa zaidi na zaidi wapambane tuu
Sabrina
Daah R.I.P Kobe jamaa alikua anajua sana huyuu
rama
:daaaa pigo sana hilii kwa mashabiki wa nba
Furahav
Daah tutamkumbuka sana.
felister
may his soul rest internal peace
Nasra
Tutakukumbuka sana
Tatu
Pengo LA Kobe alitofutika r.I.p
jullie
rip legend
Gabriel
Asiyekia la mkuu uvunjika guu tatizo aliwadharau sana wazaz wake na kujiamulia kufanya maamuz yake japo alikuwa n mchezaji mwenye mafanikio ambaye aliwakuta wakina Jordan ila aliwapita sana nakung’aa zaid but R.I.P Kobe Bryant
Asia Abdy
Ana meng mazuri yakukumbukwa
Samiah
Tutakukumbuka daima
farida ahmadi
Daima milele tutakukumbuka Kobe braynt
Latifa juma mohamed
Kobe ni mchezaji mzuri Sana pumzika kwa amani.
warda
Anastahili Kwa Kweli