Lakers inauza sehemu kubwa ya umiliki wake katika kile kinachotarajiwa kuwa mauzo ya gharama kubwa zaidi ya timu ya michezo nchini Marekani, kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mchakato huo.
Familia ya Buss imekuwa ikimiliki Lakers tangu mwaka 1979. Sasa, familia hiyo imefikia makubaliano ya kuiuza kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TWG Global, Mark Walter.
Inaripotiwa kuwa thamani ya mauzo hayo ni takriban dola bilioni 10 za Marekani (sawa na paundi bilioni 7.45), ingawa kiasi hicho kinaweza kuongezeka baada ya mchakato kukamilika rasmi.
Bw. Walter pia anamiliki sehemu kubwa ya timu ya baseball ya Los Angeles Dodgers, ambayo ilishinda Kombe la Dunia (World Series) mwaka jana.
Msemaji wa kampuni ya Bw. Walter amethibitisha kuwa mfanyabiashara huyo tajiri yuko katika hatua za makubaliano ya kununua sehemu ya umiliki wa Lakers.
“Mark Walter anaingia katika makubaliano ya kupata umiliki zaidi ndani ya timu ya NBA ya Los Angeles Lakers, ambayo tangu 2021 amekuwa na asilimia 20 ya hisa,” alisema msemaji huyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Tangu 2021, Bw. Walter amekuwa mmoja wa wamiliki wa Lakers, akiwa na asilimia 20 ya umiliki. Ana uwekezaji katika timu mbalimbali duniani, ikiwemo Klabu ya Soka ya Chelsea nchini Uingereza na timu ya mbio za magari za Cadillac Formula 1, inayotarajiwa kushiriki mashindano kuanzia 2026.
Makubaliano haya yanakuja miezi michache baada ya mauzo ya timu ya mpira wa kikapu ya Boston Celtics mnamo Machi kwa dola bilioni 6.1 kwa mfanyabiashara Bill Chisholm, ambayo wakati huo yalitajwa kuwa mauzo ya bei ghali zaidi ya timu ya michezo ya Marekani. Mauzo hayo yalizidi yale ya timu ya mpira wa miguu ya Marekani, Washington Commanders, ambayo iliuza kwa dola bilioni 6.05 mwaka 2023.
Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti Jumatano kuwa thamani ya timu ya Lakers sasa imefikia angalau dola bilioni 10. Hii inazidi rekodi za awali kwa karibu dola bilioni 4.
Jerry Buss alinunua Lakers mwaka 1979 kwa dola milioni 67.5, kwenye mkataba uliyojumuisha pia timu ya hockey ya Los Angeles Kings na ukumbi wa michezo wa Kia Forum.
Baada ya kifo cha Jerry Buss mwaka 2013, umiliki wa timu ulihamishiwa kwa watoto wake sita kupitia mfuko wa familia. Familia hiyo inamiliki asilimia 66 ya Lakers.