Ni habari njema kwa wapenzi wa mpira wa kikapu na timu ya LA Lakers. Shujaa wa Lakers – LeBron James, yupo mbioni kuongeza mkataba wa miaka miwili.

Taarifa za kuongeza mkataba mpya zimetolewa na wakala wa LeBron James ambaye aliiambia ESPN mkataba huo utamalizika 2022/23 ambapo pia James atakuwa anatimiza miaka 20 ndani ya NBA.

Mkataba mpya wa James utakuwa na thamani ya pauni milioni 63. Mwishoni mwa mkataba huu utakuwa ni mwanzo mwa safari ya mtoto wa James (Bonny – anamiaka 16 kwa sasa) ambaye atakuwa tayari kuingia kwenye NBA baada ya kumaliza masomo yake.

LeBron James, LeBron James Kuongeza Mkataba LA Lakers., Meridianbet
James Akiwa na Kombe la NBA pamoja na Tuzo Yake ya MVP.

James aliisaidia Lakers kutwaa ubingwa wa NBA mapema mwezi wa Oktoba na alibeba tuzo ya MVP katika mchezo wa fainali. LeBron James anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa NBA aliyebeba mataji ya ligi hiyo akiwa na timu 3 tofauti.

Kwa upande wa kiuchumi, kufikia mwishoni mwa mkataba wake na Lakers, James atakuwa na pato linalokadiriwa kuwa ni pauni milioni 324.

Msimu mpya wa NBA 2020/21 utazinduliwa rasmi Disemba 22 ambapo LA Lakers watachuana na LA Clippers katika mchezo wa kwanza.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

LeBron James, LeBron James Kuongeza Mkataba LA Lakers., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa