Pat Riley aliahidi miaka 30 iliyopita kwamba Miami Heat haitajijenga upya kwa kuibua vipaji, bali kwa kusaka mastaa wakubwa. Baada ya Shaquille O’Neal mwaka 2004 na LeBron James mwaka 2010, sasa ni zamu ya Giannis Antetokounmpo kuingia South Beach. Hii ni sajili ya tatu kubwa, na labda ya mwisho, kwa Riley, na inaleta matumaini mapya ya ubingwa kwa mashabiki wa Heat.

Giannis mwenyewe alieleza wazi, “Nahitaji presha katika hatua hii ya maisha yangu ya kikazi. Ili kufika kiwango kingine, lazima nitoke kwenye comfort zone, na Miami ndiyo sehemu sahihi.” Kwa kushirikiana na Bam Adebayo, Heat sasa wana timu yenye nguvu na ulinzi kwenye pande zote mbili za uwanja. Mashabiki wanaona ndoto ya taji ikikaribia tena.
Lakini tofauti na Shaq na LeBron, ujio wa Giannis unakuja na changamoto ya kiafya. Tangu msimu wa 2021-22, amefikisha mechi 70 au zaidi mara moja tu. Msimu uliopita alikosa mechi 47 kutokana na majeraha ya goti. Hata hivyo, kabla ya hapo alikuwa akipiga wastani wa 30+ pointi kwa msimu kwa miaka mitatu mfululizo, akibaki miongoni mwa wachezaji watano bora duniani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa Miami, hili ni jambo kubwa, kama Giannis atabaki imara, wanapata mfungaji na mlinzi wa kiwango cha juu. Alishinda Kia Defensive Player of the Year mwaka 2019 na ana wastani wa muda wote wa 9.9 rebounds kwa mechi. Kwa Heat, uwepo wake ni kama kufunga injini mpya inayowasha matumaini ya kurudi kileleni.

Pat Riley alifupisha kila kitu, “Giannis anataka kushinda. Kocha anataka kushinda. Mashabiki wanataka kushinda. Na huo ndiyo mpango wetu.” Sasa swali linabaki kuwa ni je afya ya Giannis itadumu? Ikiwa jibu ni ndiyo, basi Miami inaweza kuandika sura mpya ya historia ya NBA.



