Milwaukee Bucks Kwenye Mkono wa Sheria.

Kuna msemo wa kiswahili unasema ‘sheria ni msumeno, inakata pande zote’. Ndicho kilichowakuta Milwaukee Bucks kunako NBA.

Milwaukee Bucks wameingia matatani baada ya kuvunja sheria ya NBA ya kuzungumza na wachezaji huru, mlengwa akiwa ni Bogdan Bogdanovic.

Bucks waliripotiwa kuingia makubaliano na Bogdanovic mwezi uliopita licha ya mchezaji huyo kuamua kujiunga na Atlanta Hawks baada ya kufanya vizuri alipokuwa na Sacramento Kings. 

NBA wamegundua kuwa Milwaukee Bucks walivunja sheria ya muda unaoruhusiwa kufanya mazungumzo na mchezaji huru, hii imewagharimu Bucks ambao watakosa nafasi ya kuchaguliwa kwenye mzunguko wa pili 2022.

Bogdan Bogdanovic.

Taarifa kutoka NBA imeripoti “ligi ilifanyauchunguzi kama Milwaukee walifanyamazungumzo na Bogdanovic au wakala wake kuhusu mkataba wa mchezaji huru kabla ya muda unaoruhusiwa.

“Uchunguzi umethibitisha maongezi hayo kufanyika na ni uthibitisho wa kuvunjwa kwa sheria za NBA.

“Adhabu imezingatia ushiriki wa Bucks kwenye uchunguzi, kukosekana kwa ushahidi wa mkataba wowote wa awali ambao hauruhusiwi kwenye makubaliano ya mkataba kati ya Bucks na Bogdanovic na uhalisia kuwa timu haikumsajili Bogdanovic.”

Milwaukee Bucks watauanza msimu mpya wa NBA kwa mchezo dhidi ya Boston Celtics kesho Jumatano.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

12 Komentara

    Good news

    Jibu

    Duuh hatari

    Jibu

    Duu sio poa

    Jibu

    NBA wamegundua kuwa Milwaukee Bucks walivunja sheria ya muda unaoruhusiwa kufanya mazungumzo na mchezaji huru, hii imewagharimu Bucks ambao watakosa nafasi ya kuchaguliwa kwenye mzunguko wa pili 2022.

    Jibu

    Duuh pole yake

    Jibu

    Nouma Sana

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Bucks ijifunze kuendana na wachezaji

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Next time ataheshimu sheria

    Jibu

    Sio poa

    Jibu

    iko poa

    Jibu

Acha ujumbe