Michezo ya muendelezo wa msimu mpya wa NBA 2020/21 imemalizika usiku wa kuamkia leo. Boston Celtics na Philadelphia 76ers wameunga tela la Clippers na Nets.
Boston Celtics wameuanza msimu huu kwa mchezo dhidi ya Milwaukee Bucks wakati ambapo 76ers walimenyana na Westbrook Wizards.
Alikuwa ni Jayson Tatum ambaye alipeleka ushindi kwa Celtics baada ya kupachika mpira kwenye kikapu na kupata pointi 3 za ushindi wakati ikiwa imesalia sekunde 1.5 mchezo huo kumalizika.
Jayson alifunga jumla ya pointi 30 na kuchagiza ushindi wa pointi 122-121 kwa Celtics. Giannis Antetokounmpo licha ya kuwa alifunga pointi nyingi zaidi kwenye mchezo huo (35) alishindwa kutumia nafasi 2 zilizokuwa na pointi 3 kila moja wakati ilipobaki sekunde 0.4 mchezo kumalizika.

Kwingineko kunako michezo ya NBA 2020/21. Philadelphia 76ers walikuwa uwanjani wakiwakaribisha wageni wa ligi – Westbrook Wizards.
76ers waliibuka na ushindi wa pointi 113-107 dhidi ya Westbrook. Mchezaji wa kati wa 76ers – Embiid alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kumaliza mchezo kwa ‘double-double’ (pointi 29 na kucheza mipira 14 iliyokufa).
Kwa matokeo haya, Celtics na 76ers wanaungana na timu zingine zilizoanza msimu mpya wa NBA kwa ushindi.

Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumatano hii kwenye NBA 2020/21.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???




Adelta
Mchezo wa kikapu ni mzuri Sana
Ernest Kimeru
Mambo ni Moto ndani ya NBA
farida ahmad
Habari njema Sana kwa mashabiki wa NBA
Saupha mohamed
Good news
Rahmal
Mambo yametaladadi nba
Caroline
Hongera zao.
Lydia Emmanuel Magoti
Hongera zao
Issa
Wababe wapya
Hopemwaikuka
Gud to hear this
Tatu
Hongera yao
Sarah
Mambo mazuri NBA
Angelina
Goodnews
warda
Vizuri sana