Bado ni mwendo wa vuta n’kuvute kunako NBA msimu huu. Milwaukee Bucks vs Brooklyn Nets, Utah Jazz vs LA Clippers ni moto!
Baada ya kuburuta mkia katika michezo miwili ya mwanzo kunako NBA, Bucks wamerudi mchezoni kwenye mchezo wa 3. Bucks walikuwa nyumbani kuchuna na Nets ambao sasa wanaongoza kwa matokeo ya 2-1 baada ya michezo 3 kati ya 7.

Zikiwa zimesalia sekunde 11.4 kabla ya mchezo kumalizika na almanusura Bucks wapoteze mchezo wa 3 mfululizo, Jrue Holiday aliibuka shujaa kwa kupachika mpira kikapuni na mchezo kumalizika kwa mtokeo ya pointi 86-83.
Upande wa pili kunako nusu fainali ya NBA, Utah Jazz wameendelea kuwaadhibu LA Clippers kwenye Western Conference.

Donovan Mitchell alipachika jumla ya pointi 37 katika mchezo ambao Jazz wameshinda kwa pointi 117-111 na sasa wanaongoza kwa matokeo ya 2-0 baada ya michezo 2 kati ya 7.
Mchezo wa 4 kati ya Bucks vs Nets utachezwa Jumapili hii, huku Jazz na Clippers wakichuana kwa mara ya 3 Jumamosi hii kule jijini Los Angeles.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
Safi sana
Bucks wapo vizuri
Vizuri