Kabla ya kuingia uwanjani dhidi ya Houston Rockets, Golden State Warriors walikua wamepoteza michezo 6 mfululizo kwenye NBA.
Almanusura wapoteze mchezo wa 7 mfululizo, Stephen Curry ameokoa jahazi. Matokeo ya Warriors yanasuasua viwanjani. Mchezo dhidi ya Rockets, kidogo jahazi lizame kwa mara nyingine.
Kipindi cha kwanza, Warriors aliongozwa kwa pointi 54-43 lakini, walipachika pointi 33 kwenye kipindi cha 3 na kulazimisha mchezo kuingia kipindi cha nne ambacho pia, matokeo yalikua ni 76-76.
Piga ni kupige zilinogesha mchezo huu wa NBA na wakati ubao ukisoma 103-103, sekunde zikiwa zimebaki 11.5 mchezo kuisha, Garrison Matthews aliwakosesha Rockets ushindi baada ya kukosa mpira wa three pointer.
Makosa ya Matthews yakageuka kuwa faida ya Warriors ambao waliitumia nafasi hiyo kama mpira uliopotea na kwa haraka pasi ikamfikia Curry ambaye, kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake ya kucheza kikapu, alipachika mpira wa kumaliza mchezo (na ushindi) kikapuni na, ubao ukabadilika matokeo na kuwa 105-103.
Mchezo mzima ulikuwa wa aina yake. Piga ni kupige, ni kama tulikwama kwenye tope tukiwa tunaendelea kujaribu kujikwamua.
Alisema Curry baada ya mchezo.
Kwingineko kunako NBA, LA Lakers wameshinda 116-105 dhidi ya Orlando Magic, Brooklyn Nets wameshinda 117-102 dhidi ya San Antonio Spurs na Milwaukee Bucks wamewafunga 94-90 Chicago Bulls.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA