Hakika fainali ya NBA 2021 inanoga, baada ya michezo 4 kati ya 7 – matokeo ya 2-2 kati ya Milwaukee Bucks na Phoenix Suns.
Suns walikua wanaongoza kwa pointi 9 kabla ya Bucks kupindua meza na kumaliza mchezo wa 4 kwa matokeo ya pointi 103-109.
Khris Middleton alikuwa kinara wa Bucks kwa kupachika pointi 40 huku Giannis Antetokounmpo akipachika pointi 26 na kuzuia mpira ulirushwa na Deandre Ayton (Suns) kitendo kilichowapa ushindi Bucks ikiwa imesalia dakika 1 mchezo kumalizika.
Devin Booker aliwapatia Suns pointi 42 zikiwemo 18 alizopachika kwenye kipindi cha 3 cha mchezo huo. Hata hivyo, pointi za Booker hazikuwatosha Suns kufua dafu mbele ya Bucks.
Mchezo wa 5 wa fainali ya NBA utachezwa Jumapili.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!
dorophina
Walijitahidi sana bucks pongezi Kwao