NBA: Heats Yawaadhibu Lakers.

Katika muendelezo wa ligi ya NBA, Miami Heats walikuwa uwanjani wakichuana na LA Lakers. Huu ni mchezo ulioturudisha kwenye fainali ya msimu uliopita.

Lakers walipambana na Heats kwenye fainali ya NBA 2019/20 ambapo vijana wa Los Angeles waliibuka kidedea na kubeba taji hilo.

Msimu huu mambo yamekuwa tofauti, licha ya timu zote kupambana kutafuta pointi. Mipira miwili ya Jimmy Butler zikiwa zimesalia sekunde 12.4 mchezo kumalizika, iliwapa ushindi Heats kwa pointi 96-94.

Sambamba na ushindi wa Heats, Stephen Curry alikosa uhondo wa kucheza kwenye uwanja wa nyumbani wakati Golden State Warriors walipovaana na Charlotte Hornets.

Stephen Curry (wa pili kushoto) akizungumza na benchi la ufundi la Warriors kwenye mchezo dhidi ya Charlotte Hornets

Curry alikosekana kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa nyumbani msimu uliopita baada ya kuvunjika mkono.

Msimu huu, Curry alionekana akijiandaa kuingia uwanjani kuwakabili Hornets lakini baada ya muda mfupi alikaa pembeni kwa kile kilichoripotiwa kuwa hakuwa akijisikia vizuri.

Warriors walipoteza mchezo huu kwa matokeo ya pointi 102-100..


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

2 Komentara

    Heats inakuja juu sana

    Jibu

    Duu nomaaa sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.