Michezo kadhaa ya NBA imeendelea usiku wa kuamkia leo (Jumamosi). LA Lakers na Miami Heats, wamerejea mzigoni.
Baada ya kupoteza michezo yao (kabla ya wikiendi hii), hatimaye timu hizi zimeonesha uwezo wa kurejea mchezoni na kupata matokeo.
LeBron James alirejea uwanjani na kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Lakers. Vijana wa Los Angeles, walikua wakichuana na Cleveland Cavaliers. Huu ni mchezo ambao James alikua anachuana na waajiri wake wa zamani katika historia yake ndani ya NBA.

Ushindi wa pointi 113-110 kwa Lakers, umechagizwa na pointi 26 alizopachika LeBron James.
Upande wa pili, Miami Heats wameongeza wigo wa ushindi kwa kuwacharaza Charlotte Hornets kwa pointi 114-99. Tyler Herro alionesha ubora wake safari hii akitokea benchi na kupachika pointi 26.
JIUNGE KWENYE SHINDANO LETU LA EXPANSE NA USHINDE!
Achana na ndoto za usingizini za kuokota burungutu la pesa, amkia upande wa ushindi halisi kutoka Meridanbet kwenye shindano la Expanse linalojumuisha michezo pendwa ya sloti za mtandaoni iliyopo kwenye promosheni ya Expanse kutoka Meridianbet.