Kunako anga la NBA. Los Angeles Lakers wameianza vizuri hatua ya mtoano katika mchezo dhidi ya Portland Trail Blazers kwa ushindi wa pointi 111-88.

Ushindi wa LA Lakers unafanya matokeo ya miamba hii kuwa sare ya 1-1 kufuatia mchezo wao wa kwanza wa Western Conference play-offs uliochezwa katika jiji la Orlando – Florida.

Anthony Davis alikuwa shujaa wa Lakers kwa kufunga pointi 31 na kuwapatia ushindi Lakers katika mechi ya kwanza kwa mara ya kwanza msimu huu tangu mchezo wao wa nusu fainali ya mwaka 2012.

NBA
Anthony Davis

Katika mchezo huu uliokuwa wa aina yake, nyota wa Portland – Damian Lillard alivunjika kidole lakini anategemewa kucheza mchezo wao wa tatu.

Matokeo ya michezo mingine ya NBA hatua ya mtoano.

Katika mtanange wa Eastern Conference hatua ya mtoano, Milwaukee Bucks waliwafunga Orlando Magic kwa pointi 111-96 na kuwa na matokeo ya 1-1.

MVP wa Bucks kwa msimu uliopita – Giannis Antetokounmpo alifunga pointi 28 na kuweka rekodi ya kucheza mipira iliyopotea mara 20.

NBA
Giannis Antetokounmpo

Miami Heats waliwafunga Indiana Pacers kwa pointi 109-100 katika mchezo wa Eastern Conference play-off, matokeo haya yanawafaya Miami Heats kuongoza kwa ushindi wa 2-0.

Kwenye mchezo wa Western Conference, James Harden aliwaongoza Houston Rockets kwenye ushindi wa pointi 111-98 dhidi ya Oklahoma City Thunder na kuufanya huu kuwa ni ushindi wao wa pili.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi Ucheze

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa