NBA: Lakers Yatolewa Umaarufu na 76ers

Michezo kadhaa ya NBA imeendelea usiku wa kuamkia leo ambapo Mabingwa watetezi, LA Lakers, wamejikuta wakiotolewa umaarufu kwa kupoteza mchezo dhidi ya Tha Philadelphia 76ers.

Lakers walikuwa na rekodi ya kutopoteza michezo 10 waliyocheza kwenye uwanja wa ugenini mpaka sasa. Hali ilikuwa tofauti walipowafata 76ers pale Wells Fargo Center.

Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa, Lakers wakitoka nyuma kwa pointi 100-86 na kupachika pointi 13-0 zikiwa zimesalia dakika chini ya 5 mchezo kumalizika.

Baada ya vuta n’kuvute, Tobias Harris aliibuka shujaa wa 76ers baada ya kupachika pointi ya ushindi zikiwa zimesalia sekunde 2.4 mchezo kumalizika na Lakers kushuhudia kipigo cha pointi 107-106.

NBA

Kwingineko kunako muendelezo wa NBA 2020/21, James Harden na Kevin Durant wameendelea kuwa bora na kuisaidia Brooklyn Nets kuwaburuza Atlanta Hawk kwa pointi 134-128.

James Harden amekuwa mchezaji wa kwanza wa Nets kupachika pointi 30 na kutoa pasi 15 za magoli tangu Stephon Marbury alipofanya hivyo mwaka 2000.

Matokeo ya michezo ya NBA iliyochezwa Jumatano usiku: Indiana Pacers 116-106 Charlotte Hornets, Cleveland Cavaliers 122-107 Detroit Pistons, Sacramento Kings 121-107 Orlando Magic, Brooklyn Nets 132-128 Atlanta Hawks (OT), Denver Nuggets 109-82 Miami Heat, Philadelphia 76ers 107-106 Los Angeles Lakers, Milwaukee Bucks 115-108 Toronto Raptors, San Antonio Spurs 110-106 Boston Celtics, New Orleans Pelicans 124-106 Washington Wizards, Oklahoma City Thunder 102-97 Phoenix Suns, Utah Jazz 116-104 Dallas Mavericks na Golden State Warriors 123-111 Minnesota Timberwolves


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

15 Komentara

    NBA mko makini san ongeren san

    Jibu

    NBA mnatisha hongera zao

    Jibu

    NBA Mambo ni moto

    Jibu

    Lakers nao wanatuangusha sisi mashabiki

    Jibu

    Mambo 🔥🔥N B A

    Jibu

    Lakers amepoteza mchezo muhimu sana

    Jibu

    Lakers wameshuka kiwango

    Jibu

    NBA Mambo ni 🔥🔥🔥

    Jibu

    NBA noma

    Jibu

    James Harden na Kevin Durant hawa jamaa ni kisanga ndani ya NBA

    Jibu

    Lakers wametelez wapi

    Jibu

    NBA 🔥🔥

    Jibu

    Dah

    Jibu

    Nice

    Jibu

    NBA Mambo ni moto

    Jibu

Acha ujumbe