NBA: Nets Yawapiku 76ers Kibingwa.

Unapozungumzia NBA unazungumzia msimu wa kawaida ambapo ni michezo ya Eastern na Western Conference, lakini utamu wa ligi hiyo unakuwa moto kwenye hatua ya play-offs.

Michezo wa msimu wa kawaida inaendelea kutoa matokeo ya kila namna. Misimamo ya Eastern na Western Conference inabadilika kila kukicha. Hakika 2020/21 inaendelea kunoga siku baada ya siku.

Kunako michezo ya NBA iliyochezwa usiku wa kuamkia leo, Brooklyn Nets wameendelea kuwa bora kwenye Eastern Conference. Nets walikuwa uwanjani kupambana na Charlotte Hornets. Matokeo ya pointi 111-89 yaliwatosha Nets kuendelea kukaa kileleni wakifuatiwa na 76ers.

NBA
Aldridge akiitumikia Brookyln Nets kwa mara ya kwanza.

Huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa LaMarcus Aldridge ambaye amejiunga na Nets akitokea San Antonio Spurs. Aldridge alipachika pointi 11 na kutoa pasi 6 za magoli. Huu ni ushindi wa 20 kati ya michezo 23 waliyocheza Nets mpaka sasa msimu huu.

Kwingineko kwenye NBA, licha ya Golden State Warrors kuangukia pua dhidi ya Miami Heat, Stephen Curry ameendelea kuwa msaada mkubwa kwenye timu hiyo. Curry alipachika pointi 36 na kucheza mipira 11 iliyokufa.

Japokuwa wameondolewa kwenye nafasi ya kwanza, Philadelphia 76ers walimaliza mchezo wao dhidi ya Cleveland Cavaliers kwa ushindi wa pointi 114-94.


UNAWEZAJE KUKOSA KASINO YA BREAK AWAY LUCKY WILDS INAYOKUPA NAFASI YA USHINDI MURUA.

Break Away Lucky Wilds ni moja ya Sloti pendwa katika kasino za #meridianbet inayokupa mara 11,000X ya dau lako, unayo nafasi ya kuwa milionea unasubiri nini?

CHEZA HAPA

2 Komentara

    NBA wako vizuri

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

Acha ujumbe