NBA: Stephen Curry Awachoma The Bucks.

Ni mwendo wa vipigo na vicheko kunako Ligi ya NBA nchini Marekani. Rekodi zinawekwa na kuvunjwa kila iitwapo leo. 2020/21 hakika mambo ni moto!

Licha ya Golden State Warriors kutokuwa na msimu mzuri, Stephen Curry ameendelea kuwa bora na kuonesha uwezo wake binafsi katika kuitumikia timu hiyo. Warriors walikuwa uwanjani kuchuana na Milwaukee Bucks alfajiri ya leo.

Mchezo uliomalizika kwa Warriors kuibuka washindi kwa pointi 122-121, umewapunguzia machungu ya kupoteza michezo mfululizo wakati huu ambao walikuwa wameshapoteza michezo 7 kati ya 8 waliyocheza kwa siku za karibuni.

Curry alipachika jumla ya 41 huku akifunga pointi 30 katika kipindi cha pili. Warriors walipindua matokeo wakiwa wamezidiwa pointi 10 na zimesalia dakika 4 mchezo kumalizika.

Stephen Curry (katikati) akiwapa changamoto wachezaji wa Milwaukee Bucks.

“Tulihitaji ushindi ili tujisikie vizuri. Ushindi unatuongezea uwezo wa kujiamini na unatusaidia kuendelea kutengeneza utambulisho wetu.” alisema Curry.

Kwa hali ilivyo kwa sasa, Warriors wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa NBA – Western Conference na hawapo kwenye nafasi ya kucheza play-offs wakiwa wameshapoteza michezo 27 na wameshinda michezo 24.

Kwingineko kwenye NBA, Philadelphia 76ers wamerejea kwenye nafasi ya kwanza ya Eastern Conference baada ya kuwafunga Boston Celtics (106-96). LA Lakers wamewagaraza Toronto Raptors kwa pointi 110-101.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

3 Komentara

    Curry anajitahidi sana

    Jibu

    Curry. Kaza buti

    Jibu

    Pambana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.