Staa wa NBA LeBron James mchezaji wa kwanza wa mpira wa kikapu ambaye bado anacheza kuwa bilionea hii ni kwa mujibu wa jarida maarufu Forbes.
Utajiri wa nyota huyo sasa ni zaidi ya dolla za kimarekani bilioni 1 ($1b) baada ya kupata kiasi cha dola milioni 121 mwaka jana.
James ambaye ana umri wa miaka 37 amecheza misimu 19 akiwa amechezea timu kama Cleveland Cavariers, Miami Heat na Los Angeles Lakers amejipatia kwenye mshahara akiwa na timu hizo wakati zaidi milioni $900m amepata kutokana na dili za matangazo na biashara.
James anajinadaa kupata zaidi ya $44.5 kwa msimu ujao kutokana mkataba wa miaka 2 na Lakers.
“Ni hatua yangu kubwa,” alisema. “Ni wazi. Ninataka kuongeza biashara yangu. Na kama nitaipata, nikitokea kuwa mwanamichezo bilionea, ho. Hip hip hooray! Oh, Mungu wangu, nitasisimka.”
Ikumbukwe mapema mwezi huu James alisjhika nafasi ya pili kwa mwanamichezo anayelipwa pesa ndefu nyuma ya Lionel Messi ambaye alishika nafasi ya kwanza.