Nyota wa LA Lakers, LeBron James anaendelea kuweka rekodi za kipekee katika historia ya NBA.

James ambaye anashikilia rekodi ya kutwaa taji la NBA mara 4 akiwa na timu tatu tofauti, wikiendi hii alifikisha jumla ya michezo 1,300 kwenye ligi ya NBA.

LeBron James aliiongoza vyema Lakers kwenye mchezo dhidi ya Golden State Warriors inayoongozwa na hasimu wake wa muda mrefu, Stephen Curry.

LeBron James, LeBron James Afikisha Michezo 1300 ya NBA., Meridianbet
James (katikati) akipambana na wachezaji wa Warriors

Katika kusherehekea mchezo wake wa 1,300. James alipachika jumla ya pointi 19, alicheza mipira 6 iliyokufa sambamba na kutoa pasi 4 za magoli ndani ya dakika 24 alizokuwa uwanjani.

Licha ya Lakers kuendelea kumkosa nyota wao mwingine ambaye pia ni swahiba mkubwa wa James – Anthony Davis. Mabingwa watetezi wa NBA waliibuka na ushindi wa pointi 117-91 na sasa wameshinda mechi 2 mfululizo baada ya kuwa wamepoteza michezo 5 kati ya 6 waliyocheza siku za karibuni.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Huhitaji kufikiria mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

LeBron James, LeBron James Afikisha Michezo 1300 ya NBA., Meridianbet

  CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa