NBA mambo yanaeleweka huku mambo hayaeleweki ubingwa kwenda kushangilia jijini San Fransisco au Boston? kesho inawezakuwa ijumaa ya maamuzi kumaliza game 6 au Game 7 ndio itatupa bingwa.
Timu ya Golden State Warriors ikiongozwa na mastaa wake Steph Curry na Klay Thompson wanaongoza kwa kushinda michezo 3 dhidi ya 2 ya Boston Celtics, na kesho Celtics yupo kwenye dimba la nyumbani TD Garden kuweza kujitetea kwa mara ya mwisho au apigwe nyumbani.
Kwenye Game ya 5 Andrew Wiggins na Klay Thompson walikuwa wa moto ambapo kwa jumla walifunga vikapu 47 na kuisadia Golden State Warriors kuibuka na ushindi wa vikapu 104 kwa 94 na kufanikisha ushindi wao tatu kwenye NBA Final series.
Je, Celtics watalitumia vyema dimba la nyumbani na kubalance mzani na kwenda game 7 ama Steph Curry na Warriors watachukua ubingwa na kuwa mabingwa mara saba wa NBA?
NBA Fiday night ndani ya dimba la TDGarden majira ya saa kumi kwa majira ya afrika mashariki yanaenda kuamua ni San Fransisco au Boston nani atasherekea kwanza?
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.