Hatua yenye burudani kunako Ligi ya NBA huwa ni michezo ya mtoano (play-Offs). Huku ni timu 2 kuchuana mara 7, hakuna kubahatisha! Miami Heats wamefuzu hatua hiyo.
Katika muendelezo wa Eastern na Western Conferences, Heats wamefuzu hatua ya mtoano baada ya kuwafunga Boston Celtics kwa pointi 129-121. Huu ni ushindi wa 10 kati ya michezo 13 waliyocheza Heats kwa siku za karibuni.
Kuwafunga Celtics, kunawapa nafasi Heats kufuzu kwa kushika nafasi 4 kunako msimamo wa Eastern Conference. Sambamba na Heats, LA Lakers ambayo wanamkosa LeBron James kwa michezo 5 sasa, ameibuka kidedea baada ya kuwafunga New York Knicks.
Ushindi wa Lakers, unawapa matumaini ya kufuzu hatua ya Play-Off msimu huu ambao wanaingia kama mabingwa watetezi wa NBA. Ushindi wa pointi 133-104 dhidi ya Knicks, unawaweka Lakers kwenye nafasi ya 7 nyuma ya Dallas Mavericks waliopoteza mchezo dhidi ya Memphis Grizzlies.
Katika mfumo wa kawaida, timu 6 za juu kwenye misimamo ya Eastern na Western Conference zinafuzu moja kwa moja hatua ya mtoano. Timu zinazoshika nafasi ya 7-10, zitachuana kutafuta nafasi 2 zilizosalia kushiriki hatua hiyo.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Safi sana