Kunako muendelezo wa michezo ya NBA, nyota wa Golden State Warriors, Stephen Curry, ameendelea kuteka vichwa vya habari kwa uhodari wake uwanjani msimu huu.
Curry ameendelea kuwa mkombozi wa Warriors msimu huu licha ya timu hiyo kusuasua. Kwa Curry msimu huu ni mwendo wa kuweka na kuvunja rekodi. Wikiendi hii, Curry ameweka rekodi ya kupachika “three- pointers” nyingi ndani ya mwezi mmoja.
Michezo ya NBA iliyochezwa jumapili hii, Warriors walichuana na Sacramento Kings. Matokeo ya pointi 117-113 yalitosha kuwatoa kimasomaso Warriors wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Curry alimaliza mchezo huo kwa kupachika pointi 37 ikiwa ni pamoja na kupachika mipira 7 ya pointi 3 [three-pointers] na sasa amefikisha three pointers 85 ikiwa imesalia michezo 2 kumaliza mwezi Aprili.
Kwenye NBA, hii ni rekodi ambayo awali ilikuwa inashikiliwa na James Harden ambaye alipachika three pointers 82 mwezi Novemba 2019, alipokuwa anacheza kwenye timu ya Houston Rockets.

Katika michezo 14 ya mwisho, Curry amepachika pointi 30 kwenye michezo 13 akiwa na jumla ya michezo 30 aliyopachika pointi 30 au zaidi.
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Kings, kocha wa Warriors – Steve Kerr amesema “ni kama nimeishiwa maneno ya kuelezea uwezo wa Steph. Namna anavyorusha mipira, ni ubora wa kipekee”
Matokeo ya michezo mingine ya NBA:
Kevin Durant amerejea kwa kishindo kwenye timu ya Brooklyn Nets baada ya kupachika pointi 39 kwenye ushindi wa pointi 128-119 dhidi ya Phoenix Suns. Atlanta Hawks wamewafunga Milwaukee Bucks kwa pointi 111-104. Memphis Grizzlies walipindua matokeo na kuwafunga Portland Trail Blazers kwa pointi 120-113.
Charlotte Hornets wamewaadhibu Boston Celtics kwa pointi 125-104. Washington Wizards na Indiana Pacers wameendelea kujiwekea matumaini ya kucheza hatua ya mtoano baada ya kuwafunga Cleveland Cavaliers na Orlando Magic.
KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.
Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?



Magdalena
Good
Saupha mohamed
Good news
dorophina
Curry yupo vizuri
Mariam mtandama
Vizur
Adelta
Good