Sam Vincent Kujiunga APR

Bingwa wa NBA mwaka 1986, Sam Vincent, atakuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya Armée Patriotique Rwandaise (APR) kuelekea hatua ya mtoano ya Basketball Africa League (BAL) itakayofanyika Juni 6 hadi 14.

Sam Vincent Kujiunga APR

Baada ya timu yake ya South Africa’s Made By Ball (MBB) kuondolewa kwenye michuano hiyo, Vincent amepata nafasi ya muda mfupi kujiunga na APR kama kocha wa ulinzi kwa kipindi cha wiki moja ya michuano hiyo.

Sam Vincent, ambaye alishinda pete ya ubingwa wa NBA akiwa mchezaji wa Boston Celtics, anatarajia kuendelea na nafasi yake kama kocha mkuu wa MBB na kusaidia kukuza mfumo wa maendeleo ya mpira wa kikapu katika ngazi ya vijana nchini Afrika Kusini mara baada ya kumaliza majukumu yake mapya ya wiki moja.

Ukosefu wa miundombinu bora uliathiri mafanikio ya MBB mjini Kigali, ambapo walishinda michezo 2 na kupoteza 4, hivyo kuondolewa katika hatua ya awali.

Sam Vincent Kujiunga APR

Hata hivyo, timu yake ilionesha moyo wa kupambana walipoipiku APR kwenye ushindi wa 94-88. Kocha mkuu wa APR, James Maye, aliona umuhimu wa mchango wa Vincent na akaamua kumjumuisha kwenye benchi lake.

“Siku zote napenda kuwa na majukumu tofautitofauti, kwa hiyo nafurahia muunganiko huu na APR. Nafurahia kufanya kazi na kocha wao na shirika lao,” alisema Vincent, ambaye pia aliwahi kuwa kocha mkuu wa Charlotte Bobcats na kocha msaidizi wa Dallas Mavericks.

Maye na Sam Vincent pia wana mtazamo unaofanana wa kutaka kuutumia mpira wa kikapu kama chombo cha maendeleo barani Afrika. Vincent alifundisha kwa mara ya kwanza Afrika Kusini mwaka 1999, miaka 13 baada ya kushinda ubingwa wa NBA akiwa na Boston Celtics.

Sam Vincent Kujiunga APR

Sam Vincent alisema: “Mazungumzo hayo ya awali yalipelekea majadiliano zaidi kuhusu jinsi sisi kama makocha waliotoka NBA na Marekani tunaweza kushirikiana kusaidia maendeleo ya mpira wa kikapu Rwanda, Afrika Kusini, na pengine maeneo mengine ya Afrika. Nafikiri kuna dhamira ya kweli ya kuona mchezo huu ukikua, kwa sababu tunaona faida yake kwa watoto kote barani.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.