Splitter Ateuliwa Kocha Mpya wa Chicago Bulls

Chicago Bulls wameingia kwenye sura mpya baada ya kumtangaza rasmi Tiago Splitter kama kocha mkuu wa 25 katika historia ya klabu hiyo. Kocha huyo mwenye miaka 41, ambaye alikulia Brazil huku akivutiwa na Chicago Bulls ya enzi za Michael Jordan, sasa amekuja akiwa na jukumu la kuijenga upya timu hiyo inayotafuta kurudi kwenye ushindani wa juu wa NBA.

Splitter Ateuliwa Kocha Mpya wa Chicago Bulls

Splitter alikiri kuwa mapenzi yake kwa Bulls yalianzia utotoni, ambapo alikuwa akitazama michezo ya Jordan usiku wa manane akiwa Brazil, wakati mwingine akiwa mafichoni ili wazazi wake wasimkamate. Sasa, miaka mingi baadaye, ndoto hiyo imekuwa kweli kwa njia tofauti kabisa, akiwa kiongozi wa timu aliyokuwa akiishabikia akiwa mtoto.

Uteuzi wake unakuja baada ya msimu mgumu kwa Chicago ambao waliumaliza wakiwa na rekodi ya 31-51 na kushindwa kufuzu playoffs kwa mara ya nne mfululizo. Timu hiyo pia ilikuwa na moja ya safu mbaya za ulinzi ligi nzima, ikiruhusu wastani wa pointi 121.5 kwa kila mchezo, jambo ambalo limeifanya uongozi mpya kutafuta mabadiliko makubwa kuanzia benchi la ufundi.

Splitter Ateuliwa Kocha Mpya wa Chicago Bulls

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Splitter analeta uzoefu mpana katika NBA na nje ya ligi. Akiwa mchezaji, alicheza katika timu kadhaa zikiwemo San Antonio Spurs ambako alishinda ubingwa mwaka 2014. Baadaye alihudumu kama kocha msaidizi Brooklyn Nets, Houston Rockets, na pia kupata mafanikio Ulaya akiwa na Paris Basketball Club kabla ya kuiongoza Portland Trail Blazers.

Splitter Ateuliwa Kocha Mpya wa Chicago Bulls

Uongozi wa Bulls unaamini Splitter ndiye mtu sahihi kuanza ujenzi mpya, hasa kutokana na uwezo wake wa kuwasiliana na wachezaji na falsafa yake ya ushindani. Akiwa na chaguo la nne na la 15 kwenye NBA Draft pamoja na nafasi ya kutumia fedha kwenye soko la wachezaji, Splitter sasa ana kila kitu cha kuanza kuandika upya historia ya Chicago Bulls.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.