Wilson Aanza Kuwa Tishio Huko Vegas

Wakati NBA Summer League ikiendelea kushika kasi, macho yote yameelekezwa kwa kijana mpya wa Chicago Bulls, Caleb Wilson. Hata Kevin Garnett, Hall of Famer maarufu, alijitokeza kukaa kando ya uwanja akimtazama kwa makini. Garnett alimpa jina la utani la Little Ticket, akicheza na jina lake maarufu la Big Ticket. Lakini Wilson mwenyewe alisisitiza kwamba hataki kulinganishwa na Hall of Famer, bali kuandika historia yake mwenyewe. 

Wilson Aanza Kuwa Tishio Huko Vegas

Wilson alionyesha kila aina ya staili dhidi ya Los Angeles Lakers. Aliruka na kupiga dunk kali, akapiga mkwaju wa 3-point kuua maneno ya wakosoaji, akatoa pasi ya kiufundi kwa Noa Essengue, na bado akafanikiwa kuzuia layup ya Adou Thiero. Mashabiki walishangilia kama vile Vegas ilikuwa ukumbi wa muziki. Hii ilikuwa ni onyesho la kijana mwenye njaa ya mafanikio.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Wilson Aanza Kuwa Tishio Huko Vegas

Kwa takwimu, Wilson alimaliza Summer League kwa wastani wa 23.5 pointi, 7.3 rebounds, 2.5 blocks kwa dakika 27.7 tu kwa kila mechi. Alipiga nusu ya mashuti yake na 41.9% ya mitupo ya mbali. Mechi ya kwanza pekee alifunga pointi 35 na kupiga 7 kati ya 11 za 3 point. Hii siyo tu mwanzo mzuri, ni tangazo kwa NBA kwamba kijana huyu anaweza kuwa nyota wa baadaye.

Wilson Aanza Kuwa Tishio Huko Vegas

Kwa Bulls na mashabiki wao, Wilson ni mwanga mpya baada ya miaka mingi ya kusubiri. Tangu enzi za Michael Jordan, mashabiki wamekuwa wakipata maumivu na kuvunjika moyo. Sasa, pamoja na Josh Giddey, Matas Buzelis, na Norman Powell, Chicago ina msingi wa talanta na msisimko. Lakini kijana wa miaka 20 kutoka North Carolina ndiye anaanza safari ya kuandika historia yake mwenyewe.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.