Wolves Wameipata Maserati Ya NBA Kwa Kumsajili LaMelo

Mashabiki wa Minnesota Timber wolves wanapaswa kufunga mikanda yao, kwa sababu msimu huu utakuwa safari ya kasi. Baada ya kutafuta point guard wa kuongoza mashambulizi, Wolves wamepata si gari la kawaida bali Maserati ya NBA, LaMelo Ball. Akishirikiana na Anthony Edwards, hii inatarajiwa kuwa zaidi ya mstari imara wa timu kwenye ligi.

Wolves Wameipata Maserati Ya NBA Kwa Kumsajili LaMelo

Ball, aliyewahi kushinda Rookie of the Year mwaka 2021 na kuchaguliwa All-Star kabla ya Edwards, anakuja na takwimu za kuvutia, wastani wa 20.8 pointi, 7.3 assists, na 10.4 mitupo ya mbali kwa mechi katika misimu minne iliyopita. Ni playmaker, na ni mchezaji ambaye uleta tabasamu kwa mashabiki. Edwards, kwa upande wake, alimaliza msimu uliopita aliumaliza kwa rekodi bora ya maisha yake. Sasa, kwa msaada wa Ball, Edwards anaweza kurudi kwenye jukumu lake la asili la kufunga.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lakini ili kumpata Ball, Wolves walilazimika kutoa kafara kubwa ya Julius Randle na Naz Reid walioondoka kwenye dili la timu nne. Sasa kocha Chris Finch anatazamia kutumia lineup ndogo, kumhamisha Jaden McDaniels kwenye nafasi ya PF, na kumtegemea Rudy Gobert kwenye ngome ya ulinzi. Gobert, mara tisa All-Defensive na mara nne Defensive Player of the Year, anabaki kuwa mlinzi wa ukuta wa mbao na sasa anaweza kufunguliwa zaidi na Ball.

Wolves Wameipata Maserati Ya NBA Kwa Kumsajili LaMelo

Ball ana historia ya majeraha, akicheza mechi 303 kati ya 482 zinazowezekana, lakini msimu uliopita alibaki imara na kuiongoza Charlotte Hornets kufikia rekodi ya 44-38. Hata hivyo, Hornets waliamua kuanza upya, wakimtoa Ball na Miles Bridges ili kujenga kikosi kipya chenye vijana na draft picks. Kwa Wolves, hii ni fursa ya dhahabu, kumleta kijana mwenye umri wa miaka 24 ambaye anaweza kubadilisha kabisa kasi ya mashambulizi yao.

Wolves Wameipata Maserati Ya NBA Kwa Kumsajili LaMelo

Edwards na Ball wakishirikiana, Gobert akilinda, McDaniels akiongeza kasi, Wolves ambao wamekuwa wakifika playoffs mara tano mfululizo, sasa wanataka kurudi kwenye Western Conference Finals na zaidi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.