Bifu lao lilianza zamani sana katika fukwe za bata na jiji la starehe nyingi, Rio di Janeiro Brazil. Ardhi iliyofukiwa kitovu cha soka na ilipo mbingu ya miungu ya mpira.

Bebeto alicheza Flamengo na Romario alicheza Vasco da Gamma. Hawa ndio Simba na Yanga kule Rio di Janeiro, ni mbuzi na chui hawapikiki chungu kimoja.

Bebeto
Bebeto, Flamengo

Walikuwa mastaa wa timu zao na walichuana sana uwanjani. Kila mmoja alitaka kuwa bora kuliko mwingine. Wakatoana Roho kufunga.

Nje ya uwanja Bebeto alikuwa mcha Mungu, mtu anayejali familia yake kuliko pumzi yake, mtu mpole asiyekuwa na makuu na mtu.

Bebeto
Romario, Vasco da Gamma

Romario yeye alikuwa muhuni wa mtaani, mlevi na mkorofi. Utotoni mwake alitembea na bastola mfukoni ili kujihami. Ni soka lilimuokoa, pengine angekuwa jambazi sugu.

Ni Romario huyu aliyewahi kumuita Bebeto ‘Cry baby’ akisema Bebeto anapenda kuwalilia marefa ili wampendelee.

Mwaka 1994, kocha Carlos Alberto Perreira aliwaita wote ili aende nao Marekani kwenye Kombe la Dunia. Alisema Brazil ya Samba haiwezi kufanikiwa bila kuwa na Bebeto pamoja na Romario ndani.

Kabla ya kila kitu Romario aliita waandishi wa habari akawaambia hawezi kupanda ndege moja na Bebeto. Romario alikuwa akili mbili haswa, wewe msikie tu.

Ndipo kocha akawaweka chini na kuwataka wamalize tofauti zao kisha waelekeze nguvu zao Kombe la Dunia. Walikubali kupatana, kilichofuata baada ya hapo? Wapinzani walikoma kuwafahamu.

Mechi dhidi ya USA, Romario anachukua mpira kisha anaukusanya mtaa na kuondoka nao, anaingia kwenye eneo la hatari na kuweka pasi moja mguuni kwa Bebeto, Bebeto anafunga halafu anakimbia kumkumbatia Romario na kumuambia kuwa anampenda.

Bebeto

Mechi dhidi ya Uholanzi tena, Bebeto anafunga na kukimbia pembeni kisha anashangilia kama anambeba mtoto, hiyo ni baada ya kupata taarifa kuwa mke wake amejifungua.

Ghafla Mazinho ‘baba mzazi wa Thiago Alcantara’ anajumuika nae kisha Romario na yeye anajumuika kumfurahia mtoto wa Bebeto. Waliunda safu bora ya ushambuliaji.

Bebeto
Mazinho

Mwisho wa mashindano walifunga mabao nane kwa ujumla wao, Romario anakuwa mchezaji bora wa mashindano na kubwa zaidi Brazil wanabeba tena kombe la dunia baada ya miaka 24.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

bebeto, Utulivu wa Bebeto na Utukutu wa Romario, Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa