Staa aliyepata umaarufu sana kupitia soka ambaye kwa sasa anamiliki klabu yake ya Inter Miami, David Beckham alipania kuwanasa mastaa wanaotikisa ulimwengu wa soka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kutua klabuni kwake.

Staa huyu ambaye amewahi kukipiga pale LA Galaxy, mwaka jana alikuwa anafanya maandalizi ya timu yake kuingia rasmi Major League Soccer (MLS). Taarifa nyingi zilimhusisha na usajili mkubwa kwa ajili ya shughuli ambayo alikuwa nayo mbele yake.

Beckham ambaye pia amewahi kuwa staa wa Manchester United na Real Madrid, amekuwa akiweka wazi matamanio yake ya kuwanasa Christiano Ronaldo na Lionel Messi. Wote wakiwa wanafanya vyema kwenye vilabu vyao.

Beckham alikuwa anatambua ugumu wa kuzinasa saini za wachezahi hawa. Fikiria kuhusu kumuondoa Messi Barcelona au kuwashawishi Juventus kumuachia Ronaldo wakiwa wameshaanza kunogewa na kuwa naye klabuni hapo! Si rahisi!

Akiweka wazi mipango ya klabu yake na kuwazungumzia mastaa hawa, Beckham alinukuliwa akisema kuwa kila mtu huwa na mipango, orodha ya mambo ambayo anahitaji kuyatimiza.

Beckham Amewapania Messi na Ronaldo Kutua Miami
Ndoto ya Beckham ni Messi na Ronaldo Kutua Miami

Kwa upande wake ukiwaangalia Leo na CR7 wanavyocheza unawezaona kama wanakaribia kumaliza soka lao, lakini yeye haoni hivyo.

Licha ya kuwa wanacheza soka katika levo kubwa kabisa ni ngumu kuona wakiziacha klabu zao lakini beckham alisisitiza kuwa hauwezi jua nini kinaweza kutokea katika soka. Mambo mengi hayatabiriki. Hakuna mtu alijua kama Corona ingeharibu mambo mengi hadi soka, si ndiyo? Basi na Beckham aliamini hivyo.

Ni kwa mda sasa toka alivyobainisha tamanio lake la kuwanasa nguli hawa wa soka. Kimsingi hazijaripotiwa jitihada za wazi za staa huyu wa zamani kuingia sokoni kwa ajili ya mastaa wanaoshindanishwa zaidi duniani. Wenyewe wanawaita GOAT! Yaani ni wachezaji bora wa wakati wote.

Hivyo, tunaweza kujiuliza kama Beckham amekwama? Au mastaa hawa wawili hawajaweza ‘kushoboka’ na ofa yake, au ni kwa sababu timu yake ni changa bado. Niambie mtazamo wako hapa kwenye chini maoni.


Kila Mmoja Ana Namba Zake Za Bahati. Zitumie Kushinda na KENO

Cheza KENO HAPA

, Beckham Amekwama Kumnasa Messi au Ronaldo?, Meridianbet

47 MAONI

  1. kuwanasa atawanasa ila sio kwa sasa maana bado wanahitajika kwenye vilabu vyao, huko marekani wachezaji hasa hawa wakubwa hua wanaenda wakikaribia kustaafu mpira, mess na ronaldo wanamsaada sana kwa sasa vilabuni kwao!!!

  2. kuwanasa atawanasa ila sio kwa sasa maana bado wanahitajika kwenye vilabu vyao, huko marekani wachezaji hasa hawa wakubwa

  3. Beckham aendelee kukaza Buti kwani Mara nyingi mastaa upende kucheza kwa kurelax baada ya umri kwenda huenda watatua tuu kwenye Rada.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa