Beki wa kati wa klabu ya Ashanti Allies ya nchini Ghana, Hashmin Musah amekiri kuwa alijifunga magoli mawili dhidi ya Ashanti Gold kwa kukusudia kwenye mechi ya Jumamosi iliyopita ili kuharibu upangaji wa matokeo wa mechi hiyo.

Beki huyo amesema kabla ya mchezo huo, wakiwa hotelini, alisikia habari kuwa kuna ubashiri (betting) umewekwa dhidi ya timu yake ya Allies, kwamba katika mchezo huo matokeo ya mwisho yatakuwa 5-1.

 

beki, Beki Ajifunga Kuzuia Upangaji Matokeo., Meridianbet

Baada ya kusikia hivyo, akamwambia kocha wake kuwa endapo atapewa nafasi kwenye mchezo huo, ataenda kubadili matokeo hayo. Ashanti Allies waliingia katika mchezo huo wa mwisho wa msimu huu katika ligi kuu ya Ghana wakiwa tayari wameshashuka daraja.

Wakiwa wamepigwa 5-0, beki huyo Hashmin Musah alipewa nafasi ya kuingia akitokea benchi zikiwa zimebaki dakika 12 mechi kuisha. Baada ya kuingia Musah alifanya jukumu alilolipanga kwani matokeo yalikuwa 5-0 na hivyo ile Betting aliyoisikia ilikuwa inakaribia kukamilika.

 

beki, Beki Ajifunga Kuzuia Upangaji Matokeo., Meridianbet

Beki huyo alipopewa pasi aligeukia kwa kipa wake na kujifunga goli, na kurudia tena mara ya pili na hivyo matokeo kuwa 7-0. Baada ya kukamilisha kazi aliyoifuata uwanjani akafanyiwa mabadiliko kabla ya mechi kuisha.

Benchi la ufundi na wachezaji wenzake walimpongeza kwa kitendo alichofanya. Baada ya mechi Ashanti Gold walisema kuwa wao hawajahusika na suala la kupanga matokeo kama wanavyoshutumiwa huku chama cha soka cha Ghana kikiripotiwa kufungua uchunguzi.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa