Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard na mchezaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkamp wamekuwa wachezaji wawili wapya waliongezwa kwenye Hall Of Fame ya nguli wa soka la Uingereza.

Frank Lampard ameingia katika ukuta maalum wa kuwaenzi wachezaji waliocheza soka la Uingereza miaka ya 90 mpaka 2000’s kwa kiwango kizuri alichocheza kwa miaka 20 katika ligi hiyo akiwa na Chelsea. Beki wa zamani wa Arsenal pia, Dennis BergKamp amekuwa mchezaji wa sita kuongeza na kutimiza orodha ya wachezaji wa Hall of Fame.

Wachezaji hao wawili wanaungana na wenzao wanne ambao walikwisha wekwa kwenye orodha hiyo mapema mwaka huu, wachezaji hao ni  Alan Shearer, Thierry Henry, Eric Cantona na Roy Keane, ambao wote wamepigiwa kura na mashabiki na wadau wa soka duniani kote.

Lampard alicheza vizuri sana akiwa na Chelsea kwa miaka 20, lakini alipitia vilabu vya West Ham United na Manchester City kwa vipindi tofauti. Baada ya jina lake kutajwa katika Orodha hiyo, Lampard alieleza kufurahia sana na kujihisi kuwa na thamani kubwa kuwekwa katika Hall of Fame.

Nikiwa kama kijana mdogo nakumbuka nilikuwa natamani kucheza West Ham, na nilikuwa naangalia kuwa kama Roy Keane, Alan Shearer na Thierry Henry, kwahiyo kuwa katika sehemu moja na wao ni heshima kubwa sana“, alisema Lampard.

Najivunia sana na nashukuru kwa kutambuliwa. Kwangu mimi, jambo la muhimu lilikuwa ni kufanya mazoezi sana na kufanya kazi kwa bidii. Nilikuwa na talanta ya kufika na kufunga magoli. Na nilifanya hivyo katika timu zote nilizochezea na hii ilitokana na kazi nzuri na kujitolea“, alimalizia Lampard.

Kwa upande wa Bergkamp wa Arsenal ambae alichezea timu hiyo mwaka 1995 akitokea Inter, na akawasaidia kuchukua vikombe 10, ikiwemo mataji matatu ya Premier League. Akiwa na Arsenal Bergkamp, alikuwa miongoni mwa kikosi cha timu hiyo msimu wa 2003/2004, akiwa amefunga mara 87 na kutoa pasi za magoli 94, huku akicheza mara 315.

Baada ya kutajwa Bergkamp yeye alieleza kujiona wa thamani kuwa miongoni mwa kikundi kidogo cha watu waliocheza katika moja ya ligi ngumu zaidi duniani.

PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Bergkamp, Bergkamp Na Lampard Waongezwa Hall Of Fame, Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa