Kocha wa timu ya Inter Miami Phil Neville amepiga chini uvumi unaodai kwamba klabu hiyo ya Major Laegue Soccer inajaribu kuinasa saini ya staa Marcelo wa Real Madrid.
Boss wa Inter Miami Neville Amkataa Marcelo
MADRID, SPAIN – APRILI 27: Cesar Azpilicueta wa Chelsea, Marcelo wa Real Madrid wakati wa mechi ya  UEFA Champions League kati ya Real Madrid v Chelsea katika dimba la Estadio Alfredo Di Stefano  

Marcelo atakuwa nje ya mkataba mwaka 2022 lakini mchezaji huyo wa miaka 33 hatima yake haijulikani huko Bernabeu kutokana na kiwango chake kushuka miaka ya hivi karibuni.

Inter Miami ambayo inamilikiwa na staa wa zamani Real Madrid David Beckham, wameibuka na kuonesha machaguo mbadala kwa Marcelo, ambao ni Gonzalo Higuain na mshindi kombe la Dunia kiungo Blaise Matuidi kwenye kikosi chao.

Nahodha wa sasa wa Real madrid Sergio Ramos ambaye kuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huupia ameripotiwa kuwa kwenye rada za Inter Miami.

Lakini Neville amejitokeza na kupooza habari hizo za uvumi zinazo muhusisha mkongwe wa Kibrazil Marcelo na Inter Miami.

“Sidhani kama nahitaji beki wa kushoto tena,”Neville aliyewahi kuitumikia Man United aliwaambia maripota. ” Nina mabeki wa kushoto wengi kuzidi hata Tax za Njano, unaelewa nini namaanisha.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa