Saul ‘Canelo’ Alvarez na Caleb Plant wamejiandaa kukutana katika blockbuster huko Las Vegas mwezi Novemba 6.
Mpambano uliosubiriwa sana wa uzani wa kati ya bingwa anayetetea mkanda WBA, WBC na WBO Canelo na bingwa wa IBF Plant hapo awali ulikuwa umepangwa mwezi Septemba, lakini mipango hiyo ilivunjika.
Sasa, nyota wa Mexico Canelo (56-1-2) na Plant wa Amerika ambaye hajapoteza (21-0) wataingia ulingoni baadaye mwaka huu baada ya mazungumzo.
“Nimefurahi sana kuwa na pambano hili mbele yangu. Nina furaha kwa sababu nitaandika historia, na katika kazi yangu ndio hiyo ninayotaka kufanya – acha alama yangu katika ndondi,” Alvarez alisema katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi.
“Siwezi kusubiri kuona mashabiki wangu wote mwezi Novemba 6.”
Canelo alimchapa Billy Joe Saunders kwa TKO ya raundi ya nane na kuongeza idadi ya mataji ya WBA, WBC na WBO mwezi Mei.
Mbele ya mashabiki 73,216 kwenye Uwanja wa AT&T huko Arlington, Texas – umati mkubwa wa hafla ya ndondi ya ndani katika historia ya Marekani – Canelo alimchapa Saunders na kumuharibu jicho.
Canelo pia alitetea mikanda yake katika pambano la kikatili ndani ya raundi tatu dhidi ya underdog Avni Yildirim mwezi Februari.
Plant amekuwa mshindi katika mapigano yake 21 hadi sasa, rekodi ambayo inajumuisha KO 12.
Ni muda wa kuwa milionea na kasino za mtandaoni za meridianbet, mchezo wa Sahara Riches unakupa nafasi ya kushinda mkwanja mrefu. Matajiri wa jangwani wanataka wakupe mkwanja leo.