CHANGALAWE AMCHAKAZA MVENUZUELA KWA K.O

Bondia Yusuf Changalawe ameanza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kushinda pambano lake la kwanza dhidi ya Pereira Diego kutoka Venezuela kwa KO round ya kwanza, dakika ya 1 na kufanikiwa kutinga kibabe hatua ya 32 bora katika uzani wake wa Light Heavyweight 80kg katika mashindano ya kwanza ya Dunia ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024 yanayofanyika katika ukumbi wa E-Work Arena katika mji wa Busto Arsizio – Milan, Italia.

Mashindano hayo yaliyoanza rasmi siku ya Jumapili tarehe 3-03-2024, yatafikia tamati siku ya tarehe 11-03-2024.

Acha ujumbe