CHANGALAWE AMPIGA MMISRI ATINGA NUSU FAINALI

Nahodha wa kikosi cha Faru Weusi wa Ngorongoro Yusuf Changalawe amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumchakaza mpinzani wake Abdelgawwad Orabi Salah kutoka Misri kwa points 5-0.

Huu unakuwa ushindi wa pili kwa Changalawe dhidi ya mpinzani wake mkubwa katika bara la Afrika ambapo alilipiza kisasi kwa ushindi wa points 4-3 katika hatua ya 16 bora katika michezo iliyopita ya Afrika Accra 2023 mwezi March.

Mchezo wa kwanza kukutana kwa mafahari hao 2 wa Afrika katika uzani wa Light-heavyweight 80kg ilikua katika fainali ya kufuzu Olimpiki kwa Bara la Afrika 2023 katika mji wa Dakar, Senegal na Changalawe alipoteza fainali hio na kukosa nafasi ya kwanza kushiriki Olimpiki ya Paris 2024.

Mashindano haya mapya ya Mandela yatafikia tamati kwa michezo ya fainali siku ya Jumapili tarehe 21-04-2024.

Tanzania inawakilishwa na Mabondia 5, na mpaka sasa wamebakia 2 ambao ni Changalawe na Azizi Chala waliopo katika hatua ya nusu fainali.

Mabondia Ezra Paulo Mwanjwango na Abdallah Mfaume “Nachoka” walipoteza mapambano yao ya jana.

Acha ujumbe