Bingwa mtetezi wa WBC Tyson Fury amemriwa kutetea mkanda wake kwa kukabiliana dhidi ya mpinzani wa lazima Dillian Whyte, huku mpinzani huyo akitia saini kandarasi hiyo mwishoni mwa tarehe ya mwisho.

Fury vs Dillian ni Aprili 23 Ndani ya Wembely Stadium

Pambano hilo la mabondio wa uzito mkubwa linatarajiwa kufanyika mwezi wa nne tarehe 23 katika uwanja wa Wembley Stadium ambapo Fury atalipwa kiasi cha paundi milioni 24 wakati Whyte atalamba paundi milioni 6.

Promota wa Fury Warren alisema: “Tyson Fury kuja kupigana nyumbana kwenye Uwanja wa Wembley ni thawabu inayofaa kwa uzito wa juu nambari 1 ulimwenguni kufuatia ushujaa wake katika pambano lake la utatu dhidi ya Deontay Wilder.

“Ni wahusika wawili wakubwa katika mchezo wa Uingereza na wote kwa kawaida wana mengi ya kujieleza.

“Utakuwa usiku wa ajabu na tukio kubwa la michezo katika nchi hii ambalo litavutia hisia za mashabiki kote ulimwenguni.”


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa