Mike Tyson alikuwa anapigana na kibonde kutoka Ireland, Kelvin McBride. Huyu McBride alipigwa karibia na kila bondia duniani.

Alipigwa hadi na Michael Murray, bondia aliyestaafu akiwa amecheza mapambano 18 tu, alipigwa mara 17 na kushinda mara moja tu dhidi ya McBride.

McBride alikuwa kibonde kweli, na kila mtu ndani ya MCI Arena alijua atapigwa, hata McBride mwenyewe alijua atapigwa. Ila alikuja tu kupigana na Mike ili atimize ndoto zake.

Tyson alilipwa mara 10 ya hela aliyolipwa McBride. Pesa ambayo ilikwenda kulipa madeni yaliyokuwa yakimuandama.

tyson

Ukumbini alikuwepo Muhammad Alli, binadamu pekee duniani Mike Tyson anayemkubali na kumuheshimu. Aliwahi kusema wazi kuwa hamuheshimu hata mama aliyemzaa kama anavyomuheshimu Muhammad Alli.

Kabla ya kupanda ulingoni, Tyson alipata muda wa kuzungumza na Muhammad Alli. Siku hiyo hawakuzungumzia kabisa pambano, kwasababu wote wawili walijua Mike lazima atashinda.

Lakini haikuwa hivyo alipopanda ulingoni, Mike hakuwa yule aliyewahi kum-butua Larry Holmes, hakuwa yule Tyson dhidi ya Evender, hakuwa na kasi, hakuwa na maarifa.

Katika umri wa miaka 38 mwili wake haukuwa na umbo la kupigana. Ngumi zake hazikuwa nzito. Hakuwa yule Tyson aliyejulikana kama ‘the baddest man on the planet’. Alipigwa KO ya raundi ya sita.

Mike, Heshima Bora Kuliko Pesa – Mike Tyson, Meridianbet

Alishuka ulingoni anachechemea, akamuomba kocha wake awaite waandishi wa habari. Kisha kwa kinywa chake mwenyewe akasema inatosha.

“Sitakaa nipande ulingoni tena, kwasababu hii ni dhihaka kwa mchezo wa boxing. Mike Tyson si mtu wa kupigwa na mabondia kama hawa. Ni zaidi ya dhihaka kwa boxing”

Alihitimisha hivo akasema atatafuta kazi ya kufanya. Kama atakosa kazi, ni heri afe kwa njaa kuliko kuidhalilisha boxing na kweli Mike Tyson hakurudi ulingoni tena. Mpaka juzi alipokuwa na miaka 54, alicheza pambano moja lisilokuwa la ushindani na mzee mwenzake.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Mike, Heshima Bora Kuliko Pesa – Mike Tyson, Meridianbet

CHEZA HAPA

14 MAONI

  1. Hakujiandaa, alimudharau mpinzani wake,matokeo yake akapigwa. Hata hivyo Tyson anabaki kuwa bondia bora kabisa kuwahi kutokea duniani

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa