Mwakinyo Kupanda Ulingoni Kesho Jumamosi

BONDIA namba moja nchini Hassan Mwakinyo, kesho Jumamosi Septemba anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na bondia Liam Smith wa Uingereza katika ukumbi wa M&S Bank Arena ndani ya jiji la Liverpool nchini Uingereza kwenye pambano la raundi 12.

Bondia huyo atapanda ulingoni akizidiwa ubora, rekodi na uzoefu na mpinzani wake ila kama atashinda, Hassan Mwakinyo ataandika historia mpya kwenye rekodi ya ndondi duniani.

Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), Liam Smith amepigana mapambano 35 na kushinda 31, huku akipigwa mara tatu na kutoka sare mara moja tangu mwaka 2008.

Mwakinyo yeye amepigana mapambano 22, ameshinda mara 20 na kupigwa mara mbili tangu 2015.

 

Acha ujumbe