Pacquiao Anataka $40m Kuzichapa na Crawford.

Uwezekano wa Manny Pacquiao kupigana na Terence Crawford baadaye umeibuka.
Kulingana na ripoti kutoka The Daily Tribune ya Ufilipino, Pac Man tayari ameweka masharti kulingana na fedha.

Pacquiao mwenye umri wa miaka 42, ambaye alituma tweet siku chache zilizopita alifahamisha kuwa amerudi mazoezini na anatarajia pambano lake lijalo, moja ambayo itaongeza zaidi urithi wake, ameripotiwa kumtaka Bob Arum Dola milioni 40 kupambana na bingwa anayetawala ubingwa wa WBO welterweight.

“Ningependa kupigana na mtu ambaye ana jina,” Pac Man alisema kwa muandishi. “Tulimwambia Bob Arum napata dola milioni 40 na Crawford anapata dola milioni 10. Nitapambana na mtu yeyote. Unanijua; Huwa sihofii kukabiliana na yoyote. Walete. ”

Lakini Arum anaweza kusita swala la kumlipa Manny mkwanja mwingi? Dola milioni 40 ni kiasi kikubwa cha pesa. Dola milioni 50 kwa jumla itafanya pambano hilo litokee.

Neno ni kwamba pambano hili linaweza kufanyika Dubai mwezi Mei 15 ikiwa itatokea, na labda, watu wenye pesa wakikubali kulipa aina kubwa ya pesa kama hiyo huenda tukashuhudia pambano la Pac mwaka huu.


WEWE NI SHUJAA? MASHUJAA WANASHINDA HAPA!

Treasure Heroes inakupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!

Kasino ya Mtandaoni

INGIA MCHEZONI.

13 Komentara

    Mapambano hayo yatakuwa ya kishujaaa Sana

    Jibu

    Asije akataka mkwanja mrefu qrafu akachapwa

    Jibu

    Hili pambano si la kukosa

    Jibu

    Hela ndio kila kitu kwenye ulimwengu huu, hapa tatizo dau lakini Pac Man yupo tayari kupigana

    Jibu

    Mpinzani wake asije akamchapa alafu ameshabeba mkwanja mrefu wote huo wapenzi wa ndondi tunasubilia kwa hamu

    Jibu

    Mmmh mashabiki tunasubir tuone

    Jibu

    Mwamba PAC anajiamin sana

    Jibu

    Pambano kali sana

    Jibu

    Mpambano utakuwa mkali sana

    Jibu

    Huu mpambano utakuwa wa aina yake

    Jibu

    Paquiao antafuta hela

    Jibu

    Vizuri tuuu

    Jibu

    Kweli awekewe mzigo mezani

    Jibu

Acha ujumbe