Mwanamasumbwi wa Afrika ya Kusini Simiso Buthelezi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 24 siku mbili baada ya kuonekana akiwa anapiga ngumi hewani kwenye pambano lililofanyika siku ya jumapili.

Simiso Buthelezi kwenye raoundi ya mwisho alikuwa anaonekana kumzidi mpinzani wake baada ya kumuangusha chini, ghafla baada ya mwamuzi kuanza tena mchezo akaanza kuoneka kupiga ngumi upande mwengine akiwa kama mtu asiyeona au aliyepagawa na mwamuzi kumaliza mchezo.

Simiso Buthelezi

Baadae Simiso Buthelezi ilithibitka kuwa anapokea matibabu kwenye hospitali ya jijini Durban kabla ya kutangazwa kwa kifo chake siku ya jumanne.

Siku ya jumatatu mwalimu alipokwenda kumtembelea Hospitalini alisema hakuna mabadiliko kwenye hali yake, kwa sasa hajitambui, hazungumzi hajitikisi wala kufanya kitu chochote kwa sasa. Madaktari wanasema kuna uwezekano wa damu  kuvilia kwenye ubongo.

“Ni huzuni kubwa kwa wanamasumbi nchini Afrika Kusini na familia ya Buthelez kutangaza kifo cha  Simiso Buthelezi ambaye alifariki jana usiku June 7, 2022 kwenye hospitali ya Durban. Waraka ulisema.

“June 5, 2022, Buthelezi alishiriki mashindano ya ngumi ambayo yaiandaliwa na Starline Boxing Promotions, kitongoji cha Greyville, jijini  Durban. ambapo kwenye raoundi ya mwisho Buthelezi aliangauka na aliperekwa hospitalia na kugundua kuwa ana majeraha kichwani ambayo yalipelekea kuvuja kwa damu kwa ndani.

“Akiwa hospitali alipata huduma bora kadri iwezekanvyo lakini kutokana na mejara aliyoyapata ilishindikana na usiku wa alifariki dunia.”


Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa